mwanazuoni

MAJIBU YA MAKALA ILIYOPOTOSHA UKWELI KUHUSU MAHAKAMA YA KADHI.

-->
Habari ndugu JOSEPH MIHANGWA?Mimi ni miongoni mwa wadau wakubwa wa makala zako katika gazeti la RAIA MWEMA zinazoitwa NASAHA ZA MIHANGWA.Katika nakala ya gazeti hili ya tarehe 03/04/2013 uliandika mada iliyokwenda kwa jina la MAHAKAMA YA KADHI NA UZANDIKI WA WANASIA UCHARA.Kuna hoja kadha ambazo ulijaribu kuzizungumzia katika makala hii kama ifutavyo;
i)Mahakama ya kadhi na ofisi ya kadhi kugharamiwa na serikali
ii)Mahakama zetu zimepewa uwezo wa kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ubaguzi
iii)Kuruhusiwa kwa misingi ya kidinikatika jamiiya kawaida hupelekea mifarakano na mitafaruku inayoweza kutishia ustawi wa jamii.
iv)Madai ya kidini huwa na ajenda ya siriukafananisha na chui ndani ya ngozi ya kondoo na ukatoa mafano yale yaliyotokea Algeria na India.
v)Je taasisi hiyo haitaenda kudai mfumo mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi, technolojia,mabenki,bima na uhusiano wa kimataifa ili kukidhi matakwa ya sehemu moja ya jamii kwa misingi ya dini?

Kimsingi yapo mengi uliyoyazungumzia kwenye makala yako na kuyatolea ufafanuzi lakini hayo ni machache mbayo nimeona kuyatolea maelezo ili nijaribu kukufanulia na pengine utaweza kunielewa na kupata ufahamu mpana juu ya mahakama ya kadhi.Vilevile uweze kuandika vizuri juu ya hili kwa mustakabali wa taifa na watu wake.
Kwahiyo kila namba ya hoja hapo juu itawakilishwa na maelezo ya namba hiyohiyo hapa chini;

i)Kuhusu serikali kugharamia shughuli za kadhi na ofisi yake-Ni kwamba serikali kugharamia shughuli za kidini hapa nchini si mara ya kwanza wala si jambo la kushangaza ila inawezekana likawa la ajabu na la kushangaza kwa WAISLAMU,Kwasababu ni aghalabu sana kwa serikali kufanya hivyo.Unakumbuka mwaka 1992 serikali ilipo iingia mkataba na taasisi za kidini yaani TEC na CCT?Mkataba uliokenda kwa jina la MEMORANDUM OF UNDERSTANDING (MOU). Katika mkataba huo serikali inawajibika kugharamia huduma za jamii za WAIKRISTO kama vile shule za seminary na hopsitali za waikristo.Gharama zinazotolewa na serikali ni za mishahara kwa wafanya kazi, marekebisho ya taasisi hizo na mambo mengine yote ambayo yanahitajika gharama ya fedha .
Kwahiyo kuhusu gharama ya uendeshaji wa ofisi ya kadhi ni wajibu wa serikali na si swala la ajabu hapa nchini kwetu.

ii)Kuhusu uwezo wa mahakama za serikali kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ya ubaguzi-ni kweli kwamba mahakama zetu zimepewa uwezo wa kusikiliza kesi na kuamua kwa haki lakini nadhani umeshindwa kuelewa vizuri kuhusu mahakama ya kadhi , yenyewe inashughulika ndoa,talaka,mirathi na mahusiano baina ya waislamu wala haingilii watu wasiokua waislamu na haihusiki na kesi zilizonje ya hizo.
Hivyo basi kwakua serikali inaruhusu watu wake kufunga ndoa kufuatana na misingi ya dini zao basi haina budi kuwaachia raia wake uhuru wa kuendesha taratibu za ndoa zao kufuatana na misingi ya dini yao, kwasababu haiezekani ndoa ifungwe msikitini chini ya Shekhe alafu matatizo yanayohusu ndoa yakitokea yakashughulikiwe kwenye Mahakama za serikali ,badala yake matatizo yote yanayohusiana na ndoa,talaka na mirathi kwa waislamu yashughulikiwe na Kadhi.
Zipo baadhi ya nchi ambazo zina mahakama za serikali na zina uwezo wa kuendesha na kusikiliza kesi na nyengine zina idadi ndogo za waislamu lakini bado zimewapa waislamu uhuru wa kuwa na mahakama ya kadhi, Kwamfano;
*Kenya katika katiba yao ibara ya 66(3) wanaruhusu mahakama ya kadhi
*Uganada ambayo ina 12% ya waislamu lakini katika katiba yao ibara ya 129 inaruhusu mahakama ya kadhi
*Gambia katika katiba yao ya pili (1997) ibara ya 120(b) inaruhusu mahakama ya kadhi
*Nigeria katika katiba yao(Federal republic of Nigeria 1999) ibara ya 262(2) na 277 inaruhusu kadhi
Sasa hizo ni baadhi ya nchi za kiafrika ambazo pamoja na ubora wa mahakama zake lakini zimewapa uhuru waislamu wa kufuta sheria zake katika maswala ya ndoa,talaka, na mirathi .Itakua Tanzani ambayo mahakama zetu zina mlundikano wa kesi na maamuzi yasiyosthili yanayowafanya watu wasionacho ndio wahukumiwe kwa kukosa lakini mafisadi wanaoiba mabilion ya ya fedha kuishia mtaani kwa kushinda kesi je ni kweli mahakama zetu zina uwezo wa kuendesha kesi?
iii)Kuhusu mifarakano na mitafaruku inayotokana na kuanzishwa kwa misingi ya kidini -Ni kwamba matatizo hayo hayatokani tu kutokana na kuanzishwa na kwa mahakama ya kadhi bali hutokana na matatizo mengi yanayowakabili wananchi katika jamii zetu kwamfano halingumu ya maisha,matabaka kati ya walionacho na wasionacho,ukosefu wa ajira na mengine mengi,ndiyo yanayochochea wananchi kupamabana na tabaka tawala.
Lakini pia viongozi wa dini husababisha mifarakano katika jamii na mauaji kwa mfano ;Mauji ya kimbari nchini Rwanda ,waliokamatwa kwa kiasi kikubwa ni Maaskofu na wachungaji ambao ndio wachochezi wa kuu wa mauaji hayo.Walikua wakitangaza makanisani kuwa wanaostahili kuongoza ni WATUSI na si WAHUTU,hali hiyo ilipelekea wahutu wakikimbilia makanisani kuuwawa na hivyo hukimbilia Misikitini kama sehemu yao ya amani.
Vilevile umezungumzia kuhusu vita vya BIAFRA vya mwaka 1967,lakini kumbuka si tu mifarakano ya kidini ndio yaliyopelekea vita hivyo bali hata kauli za baadhi ya viongozi wa Afrika zilizokua zikichochea Kujitenga kwa taifa hilo zilipelekea vita hivyo kwamfano;Mwl. Nyerere alikuwa akichochea kujitenga kwa taifa hilo.Haya yalisemwa na Jenerali Ulimwengu katika kipindi cha Malumbano ya hoja.

iv)Kuhusu madai ya kidini kuwa na ajenda ya siri-Ni kwamba katika madai haya ya mahakama ya kadhi sisi waislamu wa Tanzania sio wa kwanza kudai bali zipo nchi nyingi ambazo zilianza kudai na kufanikisha kupata mahitaji hayo kama nilivyo kuonsha hapo juu.Na katika nchi za jirani yani Kenya na Uganda huu mfumo wa mahakama wanao na ni zaidi ya miaka 15 na haijawahi kutokea hata siku moja vurugu zilizosababishwa na uanzishwaji wa mahakama hiyo na wala ajenda yoyote ya siri ambayo imeziathiri nchi hiyo kutokana na mahakama ya kadhi. na badala yake ni amani na utulivu katika uendeshaji wa mahakama hiyo.
Kwa hiyo sisi waislmu wa Tanzania hatuna ajenda yayate ya siri kwa serikali wala taifa hili juu ya uanzishwaji wa mahakama ya kadhi ,isipokua tunataka haki yetu ya msingi katika mirathi ,ndoa na talaka.Mbona Tanzani ni miongoni mwa nchi mbili barani Afrika ambazo zina ubalozi wa Vatikan ?
Lakini nchi nyingi za kiafrika hazina ubalozi huo na waislamu wa nchi hii hatujalalamika kuwa uwepo wake ni ajenda ya siri ya KANISA KATOLIKI?
v)Hatuna haja ya kwenda kudai mfumo mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi,teknolojia na mengine ambayo umeyasema kwa sababu;
ELIMU-Tunazo shule zetu za msingi na za sekondari ambazo zinatoa elimu kulingana na mfumo wa kiislamu,sio nyingi kama za kwenu lakini hizohizo chache tunazo kwa mfano;Shule ya sekondari ya kiislamu Ubungo,Shule ya sekondari ya kiislamu Kirinjiko,Luqmani,Ridhwaa,Kinondnoni,ununio pamoja na nyengine nyingi.Vile vile tunacho Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro ambacho kinatoa elimu kwa misingi ya kiislamu,vyote ni vyombo muhimu katika kutoa elimu kwa vijana wetu kwa mfumo wa kiislamu,pia zipo taasisi nyingi za elimu ambazo zinashughulika na mfumo wa elimu ya kiislamu na elimu ya kawaida.
MABENKI NA BIMA-Pia tunazo taasisi zetu za fedha ambazo zinatoa huduma kwa misingi ya kiislamu.Kwamfano;
Amana Bank pamoja na benki nyengine za kawaida ambazo zina mfumo wa kiislamu katika baadhi ya huduma zake kwa mfano;Stanbik Bank na Natinal microfiance Bank(NMB).
SAYANSI NA TEKNOLOJIA-Pia tuna taasisi za teknolojia kama Redio za kislamu mfano;Radio Imani,Kheri,Sauti ya kuran na Tv Imani pamoja na nyengine nyingi zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika kuwaelimisha waislamu.Zipo pia Hospitali kama nile Aljumaa Hospital ya Daresalama(Karoakoo)na Ahmaddiya Hospital ya Morogoro na nyengine zikuzitaja ambazo hutoa huduma ya afya kwa waislamu na wasiokua waislamu kwa taratibu na mfumo wa dini yetu
Katika mwezi wa 03 mwaka huu ,Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alifanya ziara katika Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro ambapo alifungua jengo la sayansi na ujenzi wa jengo jipya la Teknolojia ya habari (ICT) ambalo litakapokamilika litashughulikia utoaji wa teknolojia ya habari kwa waislamu hapa nchini.
Hivyo hatuna sababu ya kiuanzisha mfumo mpya kuhusu hizo sekta ulizozitaja isipokua tunachangamoto ya kuziendeleza ili tuweze kukabiliana na changamoto za waislamu katika nchi hii pamoja na kutopata msaada kutoka serikaini lakini taratibu ishallah tutafika tunapodhamiria kufika.
Tulichokikosa sisi waislamu wa nchi ni uhuru wa kushughulikia wenyewe kesi zetu zinazohusu ndoa,talaka na mirathi kwa misingi ya uislamu.

Hivyo mi nadhani ungetumia muda wako mwingi katika kuyazungumzia matatizo ambayo watanzania yanawapata katika nchi hii.Kama vile unongozi mbaya,rushwa,maradhi,umasikini uliokithiri,ubovu wa miundombinu yetu,tatizo la ajira,huduma mbovu za afya na kufeli kwa wanafunzi wetu.Na mengineyo mengi amabyo ungewagusa watanzania moja kwa moja ,na sio kuanza kuponda mahitaji ya dini za wenzio kwani yatakupelekea kudharaulika na watu na kuonekana kama mchochezi wa vurugu za vurugu za kidini kwasababu tayari swala la mahakama ya kadhi lishakubaliwa na serikali kwani ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ,na lipo katika hatua ya awali ya utekelezaji.

ALLY AMIRI RWAMBO,
0717743549/0765394591
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment