CHAMA CHA MAPINDUZI CHAPATA PIGO JINGINE.
Aliyekuwa Diwani wa viti maalum kata ya Mbwara. Bibi Mwajabu Kingwande ( Nyakingwande) amefarikia dunia usiku wa kuamkia leo katika wilaya ya Temeke katika hospitali ya Temke.
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Katibu Uchumi na Fedha wa Tawi la Chuo Kikuu cha Waislam cha Morogoro kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Mohammed Mtulyakwaku.
alisema " Nimepokea taarifa za kifo cha Shangazi yangu bi Nyakingwande amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Temeke na Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 - 12 - 2013, katika kata ya Mbwara wilayani Rufiji napenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia msimba huu ambao ni pigo kwa familia na wana ccm wa kata, wilaya(Rufiji) na nchi kwa ujumla"
Bibi Nyakingwande ni mzarendo wa kuigwa ndani ya nchi hii kwani alikuwa mpambanaji mkubwa ndani ya kata ya Mbwara na Wilaya ya Rufiji kwa ujumla kua kikisha CCM ina shinda katika nyanja zote kwa kua alikipenda sana CHAMA CHA MAPINDUZI kutoka moyoni . Napenda kuwapa pole wana CCM wote wa nchini Tanzania .
0 comments:
Post a Comment