MBUNGE JOSHUA NASSARI AMKACHA MHE: HALIMA MDEE
Mbunge Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari amefunga ndoa na Anande Nko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru jijini Arusha ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto.
Sherehe hiyo ilianza mishale ya saa 7:00 mchana siku ya leo ambapo watu wote walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru Mashariki ambao wamepiga ‘mpunga’ wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu akaondoka akisema ‘Nassari ameacha historia’.
Tanbih: Mbunge huyu alisema kuwa atamuoa Halima Mdee wakati wanafanya kampeni katika jimbo la Arumeru hii ni ndio sababu ya mwandishi kusema kuwa Mbunge huyu amemkacha Mhe: Halima James Mdee.
0 comments:
Post a Comment