mwanazuoni

WATU 17 WADAIWA KUFARIKI KATIKA AJALI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA








Watu  zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa  baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katika kijiji  cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.


Ajali hiyo imetokea leo  majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda  Mwanza kugongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda. Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.
Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo na kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi (Day-worker)

Baadhi ya miili ya marehemu.Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment