Ili tuendelee
tunahitaji vitu vikuu vine; Watu, Ardhi, Siasa
safi na Uongozi bora (Azimio la Arusha 1967). Siasa safi ni kichocheo cha
maendeleo. Ni utaratibu ambao watu katika nchi hujadili changamoto
zinazowakabili na kupendekeza namna ya kuzitatua kwa nguvu ya hoja huku
wakisisitiza umuhimu wa upendo, Amani na ustawi wa pamoja. Ni utaratibu ambao
wagombea wa viti mbalimbali watashindanishwa kwa sifa, uwezo, uzoefu, hekima,
busara na maalifa waliyonayo. Ni utaratibu mzuri unaowezesha kupata viongozi
bila kueneza chuki, hila, majungu, udini, ukabila wala fitina miongoni mwa
jamii. Ndio njia pekee ya kuliwezesha Tafa kupata viongozi bora katika hali ya
Amani na mshikamano wa Kitaifa. Siasa chafu ni ile ambayo vyama vya siasa
hudiliki kuandaa mikakati ya kuwagombanisha wananchi ili viweze kupata fulsa ya
kutawala. Vipo tayari kuandaa mikakati ya kupoteza uhai wa baadhi ya wananchi
ili viweze kuchaguliwa kushika dola. Ni Siasa za makundi, za kirasimu na
kutumia pesa. Siasa ambazo Vyama vya siasa vinatafuta ushindi kwa gharama
zozote pasipokuzungatia demokrasia huru na makini. Siasa chafu zimefanya watu
waone ya kwamba siasa ni uwanja wa fujo na sio mfumo wa kuwawezesha kupata
viongozi bora kwa njia ya Amani. Mchakato wa uchaguzi ndani na nje ya vyama
shindani na katika taifa zima umetoa mwanya kwa wanasiasa kutumia mbinu zote
wanazozijua ili kujipatia ushindi katika mfumo a vyama vingi vya siasa. Ushindani
wa kisiasa uliopo umebaini hisia za kidini, ukabila, matumizi ya mabavu,
ukanda, utofauti wa rika (vijana na wazee) na vita vya kisiasa vya wenyewe kwa
wenyewe miongoni mwa wanachama wa chama husika na wananchi kwa ujumla. Taratibu
za kampeni na uchaguzi zimekuwa ni za kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe na pia
kuhujumu demokrasia. Wagombea wanapandikiza chuki na kuwagawa wananchi ndani ya
vyama na nje ya vyama ili kupitia mgawanyiko huo wapate mwanya wa kutawala.
Wagombea wanadiliki kununua wapiga kura na hata kuandaa mkakati maalumu wa
baadhi ya watu kupiga kura zaidi ya mara moja. Utaratibu wa namna hii hauwezi
kujenga Taifa imara, siasa safi haipaswi kutoa mwanya kwa wagombea au vyama vya
siasa kutumia mbinu hata zile zinazohatarisha uhai wa wananchi na Taifa..
- Je Taifa letu linaendesha siasa safi?
- Je vyama vyetu vya siasa vinaendesha siasa safi?
- Je hatuoni sababu ya kuja na azimio lenye lengo la kujadili kwa kina maana na namna ya utekelezaji wa siasa safi, mapungufu ya demokrasia ya sasa na maana halisi ya demokrasia?
Raisi wa Marekani
Abraham Licon aliwahi kusema ya kwamba’Demokrasia ni Serikali inayoundwa na
kuongozwa na watu kwa ajili ya watu’ Lakini Serikali nyingi leo hususani katika
Bara letu la Afrika zinaundwa na watu lakini haziwanufaishi watu isipokuwa
tabaka tawala. Tabaka tawala linaishi maisha mazuri, ya kupendeza na kutamanika
lakini tabaka la wapiga kura. tabaka la watawaliwa linaendelea kuwa masikini
siku baada ya siku.Utekelezaji wa demokrasia ni tofauti kabisa na demokrasia
yenyewe. Hakuna mtu anaehitaji demokrasia ambayo sauti ya wanyonge haisikilizwi
na wala ikisikilizwa haithaminiiwi. Demokrasia halisi hailuhusu kuwepo kwa
matabaka kati ya wenye nacho na wasionacho. Demokrasia halisi inaamini ya
kwamba binadamu wote ni sawa hivyo wanastahli thamani inayolingana. Jamani kama
utekelezaji wa demokrasia ni tofauti kabisa na maana halisi ya demokrasia
hakuna sababu za kuendelea na utekelezaji wa demokrasia usiokidhi demokrasia
yenyewe. Utekelezaji wa demokrasia unaokizana na maana halisi ya demokrasia
unatokana na viongozi dhaifu waliopatikana kwa siasa chafu.
Tanzania ipo katika kipindi
ambacho uongozi umeonekana hauna maana, haufai kutokana na kushindwa kutatua
changamoto za watu kwa wakati. Watu wanaona ni bora waishi pasipo na viongozi
kutokana na umuhimu wa viongozi kutokuonekana.Yote haya yamesababishwa na siasa
chafu zinazotumika kuwaweka viongozi madarakani.
Nitumie fulsa hii kutoa wito
kwa Watanzania wenzangu; kuangalia namna ya kuishinikiza Serikali na Bunge
kutunga sharia na utaratibu utakaowezesha uendeshaji wa Siasa safi ili tuweze
kupata viongozi bora. Kiandaliwe kitabu kinachoelezea namna ya kutekeleza siasa
safi katika nchi yetu
Tegemeo Sambili 0717250797
0 comments:
Post a Comment