Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) lililoahirishwa katika jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani hivi karibuni sasa litafanyika kuanzia Julai 7-20 kwa mkoa wa Pwani na Julai 16- 25 kwa jiji la Dar es salaam.
Uboreshaji
wa Daftari hilo kwa jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani uliahirishwa
kutokana na kuchelewa kwa vifaa vya uboreshaji kutoka mikoani ambavyo
vilipelekwa ili kuongeza ufanisi kutokana na maeneo hayo kuwa na idadi
kubwa ya watu wenye sifa ya kuandikishwa kuwa Wapiga Kura.
Mkurugenzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Mallaba amewataka wananchi wote wa
mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya uandikishaji
vitakavyokuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa ili kujiandikisha
waweze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka katika Uchaguzi
Mkuu Mwezi Oktoba Mwaka huu.
Amewataja
watakaohusika na zoezi hili kuwa ni watu wote waliotimiza umri wa Miaka
18 na kuendelea na wale watakaotimiza Miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba
Mwaka huu.
Wengine
ni waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la
zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
Aidha Mallaba amewataja wengine wenye sifa ya kujiandikisha kuwa ni wale
wote wenye sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye
Daftari hilo.
Amesema
wale wote wenye Kadi za kupigia Kura za zamani wanatakiwa kwenda na
Kadi zao ili kurahisisha uchukuaji wa taarifa zao na kadi hizo
zitarudishwa NEC na watapata vitambulisho vipya. Wananchi wanatakiwa
kujiandikisha katika Vituo vilivyopo ndani ya Kata zao ili kuweza kupata
fursa ya kumchagua Diwani, Mbunge na Rais.
Mkurugenzi
huyo ametoa wito kwa wananchi wa mikoa hiyo kuhakikisha wanajiandikisha
kwani bila kufanya hivyo hawataweza kupiga Kura wakati wa Uchaguzi
Mkuu. Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00
asubuhi na kufungwa ifikapo saa 12:00 jioni.
0 comments:
Post a Comment