Habari zenu ndugu zangu! Bila shaka m'buheri wa afya. Leo nahitaji kuzungumzia suala zima la Umuhimu wa ELIMU. Kwani nyote mnafahamu kuwa Elimu Ni Ufunguo wa Maisha(Maendeleo). Ila sina haja ya kwenda Mbali sana kwa lengo la kutoa mifano juu ya Mafanikio ya Elimu kwani Mwenye Macho Haambiwi Tazama.
Kwa kutambua Umuhimu wa Elimu Bora, Mheshimiwa Diwani wa Kata Ya MIJELEJELE Ndugu Juma Polle , Leo Siku Ya Jumanne Tarehe 12/01/2016. Mnamo saa 4 asubuh atakabidhi VIFAA VYA SHULE kama vile :
a. Mabegi ya shule
b. Madaftari
c. Rula, Peni.
d. Sare za Shule, soksi na mikebe.
Kwa wanafunzi wanne wa kidato cha Kwanza ambao ni:
1. Chiunda Bakari Chiunda
2. Nashru James Lameck
3. Joseph Charles na
4. Ezra Simon Halfan
NB: Vifaa hivyo vitatolewa katika Ofisi Ya Diwani Kata Ya MIJELEJELE Ndugu JUMA POLLE
Mwandishi.
Mshana Junior
12/01/2016
Diwani Juma Polle |
0 comments:
Post a Comment