mwanazuoni

MWIGULU NCHEMBA APASUA JIPU LA UFISADI KATIKA MACHINJIO YA VIGUNGUTI


WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ACHUKUA HATUA HIZI HAPA,BAADA YA KUKUTANA NA UFISADI MWINGINE NDANI MACHINJIO YA VIGUNGUTI.
Nimerejea asubuhi ya leo kwenye machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili watumiaji(wadau) wa machinjio hayo.
Kutokana na uwepo wa ubadhilifu wa kodi ya serikali kwenye mnada wa pugu na malalamiko kadhaa yanayogusa wananchi wanaotumia machinjio haya,Nimeshirikisha wizara mbili(TAMISEMI na AFYA) kutoa majawabu ya muda mfupi na yakudumu.Haya ndio maamuzi tuliyofikia.

1.NImeagiza kuwa Mkuu wa mnada wa pugu na Watumishi waliokuwa zamu tar.24.12.2015 na tar.01.01.2016 kuanzia sasa watafute kazi nyigine,wakati huohuo wahakikishe wanafika ofisi ya Katibu mkuu wizarani kwangu mapema Jumatatu tar.04/01/2016
2.Kuanzia sasa nimesitisha uchukuaji wa Ushuru eneo la mnada wa pugu,badala yake makusanyo yote ya fedha za serikali hizo yatafanyika Machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine za Elektroniki za EFD,Kwa maana hiyo mnada wa pugu utakuwa unatumika kutoa vibali tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa mifugo inayopaswa kuchinjwa.
3.Eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa limejengwa kwa fedha za Wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe kwaajili ya Wananchi kulitumia kuhifadhia nyama hiyo,Awali eneo hilo lilifungwa bila sababu za msingi.Vilevile umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo urudishwe hii leo kwaajili ya kuwarahisishia wananchi shughuli zao.
Hatua za kuboresha miundombinu ya Machinjio hayo zimeelekezwa kwa Halmashauri ya Ilala zifanyiwe kazi haraka na kwa ubora.


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment