Boniphace Jacob, Meya wa Manispaa hiyo leo amesema, awali alifanya
ziara katika maeneo hayo na kuzungumza na wafanyabiashara ambapo
aliwataka kutofanya biashara zao kwenye eneo la Ubungo na badala yake
kuhamia Mawasiliano.
“Soko hili ni kwa ajili yenu nyie wamachinga, mama lishe kila mwenye
biashara aangalie kunakomfaa na kufanya biashara, kila mtu atapewa
kitambulisho kutoka manispaa kimtambulishe eneo lake husika,”amesema.
Amesema, aliona si busara kuwaondoa wafanyabiashara hao bila kuwa na maeneo ya kwenda kufanya biashara zao.
“Niliomba wiki mbili kamati ya ulinzi na usalama ya kinondoni
msivunjiwe hadi hapo nitakapowatafutia eneo la kufanya biashara zenu, ni
jukumu langu kujua mtakwenda wapi. Kuanzia leo, atakayekuwa Ubungo
asinisumbue, watu wangu wako salama mawasiliano,” amesema.
Na kwamba, hatarajii kuona Jeshi la Polisi au mgambo wanawasumbua
wafanyabiashara hao huku akiwaomba kuacha njia kwa wanunuzi watakaofika
sokoni hapo.
“Hakuna atakayekosa eneo la kufanyia biashara hapa, kila mtu atapata
wauza mabegi ule uzio upendeze kwa kutundika mabegi na wauza nguo pia,
lakini pia msilipe ushuru kwa mwezi mmoja baada ya mwezi mmoja ndiyo
mtalipa,” amesema.
Meya huyo amesema, wafanyabiashara ambao tayari wamepanga biashara
zao wasibugudhiwe, waliopewa na kutofanya biashara wapewe watu wengine
wafanye.
Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakiwahi nafasi katika eneo hilo,
walilalamika kwa wengine kutopata kwani tayari eneo limeonekana kuwa
dogo.
Husna Khamis na Amida Juma ni miongoni mwa wafanyabiashara ambao
wamesema, wana wasiwasi na maeneo hayo kutopata kwani waliowahi maeneo
hayo asilimia kubwa si wafanyabiashara waliopaswa kuondoka Ubungo.
“Mimi sijapata eneo unavyoniona hapa, kila ninapoangalia naona majani
watu wamewahi, ingawa Meya ametuambia tuweke biashara kama eneo halina
mtu, ukienda ndani wanakuambi ulipe sh 140,000 ndiyo upate,” amesema
Juma.
Awali Jacob alisema, maeneo hayo yamegaiwa bure huku akisisitiza mtu
atakayeuza atachukuliwa hatua pamoja na kunyang’anywa eneo husika na
kupewa mtu mwingine.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

Mtani
0 comments:
Post a Comment