Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki
wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya
mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za
mwisho.
Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada
ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo
kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo
mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba.Mwanahabari wa BBC Tamasin
Ford anasema kuwa mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi na kubeba
mishumaa ili kutoa heshima kwa nguli huyo wa muziki.
Mkewe Papa Wemba na wasaidizi wake pia walikuwepo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment