Mahakama
ya Rufaa imesikiliza rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu
wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es salaam ‘RCO’ Kamishna Msaidizi wa Polisi
‘ACP‘ Abdallah Zombe na askari wenzake watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Rufaa hiyo
imesikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu ambapo wamesikiliza pande
zote mbili wa mashitaka na utetezi na itatoa maamuzi baada ya majaji
kupitia kesi hiyo.
Mkurugenzi
wa Mashitaka ‘DPP’ alikata rufaa mwaka 2013 akipinga hukumu ya Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es salaam iliyowaachia huru Zombe na wenzake baada ya
kuwaona hawana hatia katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa
inawakabili.Aliyewahi kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar es Salaam kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake watatu leo wamefikishwa mahakama ya Rufaa ambapo mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali 'DPP' anapinga kuachiwa huru kwao baada ya kushinda mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili ya mauaji. Mahakama ya Rufaa imesikiliza pande zote mbili na itatoa maamuzi baada ya majaji kupitia kesi yote.

Mtani
0 comments:
Post a Comment