Bao lililofungwa na Danielle carter lilikisaidia kikosi cha wanawake wa timu ya Arsenal kuchukua taji la 14 la kombe la FA baada ya kutawala mechi dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley.
Carter,ambaye alipiga juu alipopata nafasi yake ya kwanza aliipatia the Gunners uongozi baada ya kuvamia lango la Chelsea.
Asisat Oshoal baadaye alikosa fursa tatu za wazi kuongeza ushindi huo wa Arsenal.
Fran Kirby alipoteza nafasi ya wazi ya kusawazisha kutoka upande wa Chelsea katika mechi ya fainali iliohudhuriwa na mashabiki 32,912.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza alikosa mwelekeo katika kipindi cha kwanza na hivyobasi kumpatia fursa kipa sari Van Veenendaal kuokoa mikwaju yake. BBC
0 comments:
Post a Comment