Klabu ya Norwich City imeshushwa daraja kutoka Ligi ya Premia licha ya kuandikisha ushindi dhidi ya Watford.
Klabu ya Newcastle United pia imeshushwa daraja.Ushindi wa Sunderland wa 3-0 dhidi ya Everton Jumanne uliwafikisha hadi alama 38 na kwa kuwa Norwich na Newcastle hawawezi kuwafikia, moja kwa moja klabu hizo mbili zikashushwa daraja.
Kwa sasa Norwich wana alama 34 sawa na Newcastle. Klabu nyingine iliyoshushwa daraja ni Aston Villa iliyo na alama 17 kwa sasa.
Troy Deeney alikuwa amewapa Watford uongozi mechi hiyo iliyochezewa Carrow Road lakini Norwich wakajibu kupitia bao la Nathan Redmond.
Dieumerci Mbokani aliwafungia Norwich la pili naye Craig Cathcart akawaongezea la tatu kwa kujifunga.
Odion Ighalo alikomboa bao la pili lakini Mbokani akawafungia Norwich bao la nne.
Baada ya kushushwa daraja, Norwich sasa watakuwa wakichezea tu fahari mechi yao ya mwisho dhidi ya Everton Jumapili.
Watford watajaribu kumaliza msimu vyema dhidi ya Sunderland nyumbani.
0 comments:
Post a Comment