Mgombea anaewania urais nchini
Marekani Donald Trump ameonya kuwa henda asiwe na uhusiano mzuri sana na
waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron -- Ikiwa atakuwa rais wa
Marekani.
Mwezi Disemmba, Bwana Cameron alimtaja Trump kama mtu
mwenye "ubaguzi, mjinga, na mwenye makosa" kufuatia kauli yake kwamba
ataweka marufuku ya muda ya kuingia Marekani dhidi ya waislam.Bwana Cameron amekataa kufuta kauli zake dhidi ya Bilionea Trump , ambae anatarajiwa kuwa mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican katika uchaguzi wa mwezi Novemba.
Kuhusu kauli za Bwana Cameron, Bwana Trump alisema : "yaelekea hatutakuwa na uhusiano mzuri sana, nani anajua.
"natumai kuwa na uhusiano mwema na yeye, lakini inaonekana ni kama hataki kutatua tatizo."
Donald Trump pia alimkemea Meya wa London , Sadiq Khan, kwa kumuita "mjinga".
Alielezea kauli yake kama kosa na isiyokua na ya heshma, huku akimtaka Bwana Khan afanyiwe vipimo vya uwezo wa akili yake (IQ).BBC
0 comments:
Post a Comment