Kiwiliwili cha bwana Sankari' kimepatikana kimetupwa mjini Instabul |
Mwanaume mmoja mpenzi wa jinsia moja raia wa Syria amechinjwa na kiwiliwili chake kutupwa mjini Instabul Uturuki.
Kichwa chake hakijulikani kilipo.
Hata hivyo wapiganiaji haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Uturuki wameutambua kiwiliwili hicho cha raia huyo wa Syria huku wakisema kuwa alikuwa ameteswa kabla ya kuchinjwa.
Wapenziwe mtu huyo wanasema kuwa majuzi tu alikuwa ameshikwa na watu wasiojulikana na kubakwa na kundi la watu.
Kwa mujibu wa washirika wake Muhammad Wisam Sankari alikuwa ametishiwa maisha mara kadhaa na makundi ya wanaume.
Wameiambia shirika moja la kutetea haki zao kaosgl.org, kuwa maisha yao yamo hatarini.
Sankari, aliwasili Uturuki mwaka uliopita na alikuwa akiishi katika mji wa Instabul kabla ya kiwiliwili chake kupatikana katika mitaa ya Yenikapi mnamo julai tarehe 25.
Kaosgl.org, inasema kuwa Sankari alijaribu kuomba uhifadhi katika mataifa mengine baada ya kubakwa yapata miezi mitano iliyopita.
''Tulijaribu kuomba msaada wa ulinzi wa polisi baada yake kutekwa na kisha kubakwa miezi mitano iliyopita lakini hatukufaulu kupata chochote''
Rafiki wa karibu wa marehemu Diya, anailaumu umoja wa mataifa kwa kushindwa kuwalinda watu wa jamii hiyo yao.
''Kila mara wanapokutaka nawe uwe hujapenda huwa wanakuandama na kukutoa uhai''
Mwandishi wa BBC aliyeko Uturuki Cagil Kasapoglu amesema kuwa mashambulizi mengi dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja huwa hayaripotiwi kwa vyombo vya dola.
Kumekuwa na visa 5 vya mauaji ya wapenzi wa jinsia moja na mashambulizi 32 mwaka uliopita.
Katika wakati huohuo watu 3 walipatikana wamejitia kitanzi.bbc
0 comments:
Post a Comment