Simba ilishinda tena mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Burkina Faso, mchezo huo uliochezwa jana jioni ulimalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 5-0.
Magoli ya Simba yamefungwa na Ibrahimu Ajibu dakika ya 1 na dakika ya 35, Mussa Ndusha Dakika ya 15′ Shizya Kichuya dakika ya 55 na Said Ndemala dakika ya 65 mchezo huu ni wa tatu kwa timu ya Simba kupata ushindi katika michezo yote mitatu ya kirafiki aliyocheza tangua iweke kambi mkoani Morogoro.
Imeshacheza na Timu ya Polisi Moro wakapata ushindi wa 5-0,Simba vs Moro Kids ikashinda kwa goli 2-0. Simba inatarajia kucheza mchezo mwingine wa kirafiki siku ya Jumatano dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni na kujiandaa kurud Dar kwa ajili ya Simba day August 8.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment