Mhe.Tundu Lissu amepandishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu saa 8:56 mchana kwa tuhuma za uchochezi. Pichani ni baadhi ya viongozi wa CHADEMA, wanachama pamoja na mawakili waliomsindikiza mahakamani hapo.
Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa Julius Mwita amekamatwa na polisi akiwa Mahakamani hapo alipokwenda na wenzie kumsindiza Lissu.
Wakati huohuo taarifa kutoka Singida zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo limetoa hati ya kukamatwa kwa Tundu Lissu kwa madai ya kutoa lugha ya uchochezi wakati akifanya mkutano wa hadhara mkoani humo jumatano ya August 03, 2016.
UPDATES
Mawakili wa Serikali wameiomba Mahakama imzuie Peter Kibatala kuwa wakili wa Tundu Lissu. Hakimu amesimamisha kesi kwa muda ili wajadiliane chamber kujua kama ombi hili la mawakili wa serikali ni valid kisheria.!
UPDATES..
Manawa Bukwimba nae amekamatwa mahakamani Kisutu na jeshi la Polisi alipokwenda kusikiliza kesi ya Lissu. Haijafahamika Polisi wamempeleka wapi. Ufuatiliaji utafanyika baada ya kutoka Mahakamani.!
Manawa Bukwimba nae amekamatwa mahakamani Kisutu na jeshi la Polisi alipokwenda kusikiliza kesi ya Lissu. Haijafahamika Polisi wamempeleka wapi. Ufuatiliaji utafanyika baada ya kutoka Mahakamani.!
UPDATES.!!
Mawakili wa Serikali wamemuomba Hakimu ili Peter Kibatala awe shahidi upande wa Jamhuri badala ya kuwa Wakili wa Lissu. Upande wa Jamhuri umesema Kibatala anapaswa kuwa shahidi wao maana anajua statement aliyoisema Lissu na alikwepo wakati maneno hayo yakitamkwa. Hivyo kwa mujibu wa sheria hawezi kuwa Wakili wa Lissu na baadae akawa tena shahidi wa jamuhuri.
Kibatala amewaambi amekataa ombi hilo la Jamhuri na kusema "Mnanilazimisha niwe shahidi wenu!?? Siyajui hayo maneno na sikuwepo wakati huo mnaodai Lissu aliyasema"
Hakimu amekataa ombi la Upande wa Jamhuri la kutaka kumtumia Kibatala kama shahidi wao kwa kuwa hoja yao haina mashiko.!
UPDATES:
JAMHURI: Tunaiomba Mahakama kama Mawakili wa Serikali Wakili msomi Kibatala akae pembeni kwakuwa ni shahidi wetu kwa hatua za baadae. Sisi Mawakili wa Serikali hatupingi Kibatala kuwa Wakili wa Lissu tunachopinga ni kwamba baadae tutamuhitaji awe shahidi na mteja wake atakosa mtetezi.
KIBATALA: Mheshimiwa Hakimu hiyo huruma ya upande wa jamuhuri juu ya mteja wangu imeanza lini?? Kama shauri hili hutaweza kuliamua twende Mahakama Kuu ifanye maamuzi.
Mawakili wa Serikali wanatoa hoja ya pingamizi la dhamana kwa mshtakiwa. Wamewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa Lissu. Katika hati hiyo imeeleza namna ambavyo mshitakiwa akiwa nje kwa dhamana ataathiri upelelezi.
JAMHURI: Mheshimiwa Hakimu mshitakiwa amefanya
makosa mawili mfululizo na tabia hii inaweza kuwa kigezo cha msingi kumnyima mshitakiwa dhamana. Rejea kesi ya S/Maharaji ya Mwaka 1976. Wakili wa serikali anatala kusoma kifungu hicho...
HAKIMU: Usisome, nitasoma mwenyewe okoa muda.
JAMHURI: Mheshimiwa Hakimu mtu wa aina ya Lissu yeye mwenyewe kwa kurudia kosa amejinyima haki yake ya msingi ya dhamana....!
Kwa hisani ya Edward Simbey
UPDATES.!
Upande wa Jamhuri umemaliza kuwasilisha, sasa ni upande wa mshtakiwa.
KIBATALA: Mheshimiwa Hakimu sisi tunaomba mteja wetu apewe dhamana. (Mawakili wa Jamhuri wanaingilia kati. Wanapinga Kibatala kumtetea Lissu maana watamtumia kama shahidi baadae).
Lissu anasimama.....
LISSU: Mheshimiwa Hakimu, Wakili Kibatala ni wakili wangu, na hakuna sheria inayomzuia kunitetea. Lakini kama upande wa Jamhuri hautaki anitetee basi nitajitetea mwenyewe...
Hakimu anamruhusu Lissu kujitetea.
Lissu kaomba hati ya kiapo na vitabu vya sheria. Mawakili wa Serikali wote wamesimama na wanapinga Lissu kujitetea. Hakimu anawataka wakae chini. Lissu kaambiwa aendelee....
Kwa hisani ya Edward Simbey
UPDATES.!
LISSU: Mheshimiwa Hakimu naomba nijibu hoja za kupinga dhamana zilizotolewa na upande wa Jamhuri dhidi yangu. Mheshimiwa naomba nianze na kiapo iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri mbele yako. Mheshimiwa Hakimu Kiapo ambacho kipo mbele yako hakina Tarehe ya kiapo chenyewe na hakuna anuani. Hivyo kiapo hiki si halali..
Kifungu cha 8 cha sheria za viapo kinasema kwamba kila Kamishna wa viapo atataja kwa Ukweli mahali kiapo hicho kilipotolewa na Tarehe ya kiapo hicho. Mheshimiwa Hakimu, Mahakama zetu za juu katika kesi mbalimbali wamesema kamishna wa viapo lazima aoneshe anuani na lazima aandike tarehe. Kiapo hiki hakina anuani wala hakina tarehe bali kina muhuri. Laakini sheria inasema muhuri sio uhalali wa kiapo. Kwa hiyo naomba kiapo hiki usingalie kabisa. Na ukiona kinafaa kuangalia kwa hoja zilizotolea basi fanya na haya yafuatayo....
HAKIMU: Mheshimiwa Lissu endelea...
LISSU: Mheshimiwa Hakimu aya ya 7 na ya 8 ya kiapo inaelezwa kwamba ninyimwe dhamana kwa ushahidi ambao Mahakama yako haijui. Wanataka niende magereza kwa hati ambayo haina uhalali. Na wanajua haina uhalali ndio maana wakaandika kwenye kiapo disclosed kwasababu kina hoja za kuungaunga. Mheshimiwa Hakimu naomba usikubali kuingizwa katika mtego huu..
Kwa hisani ya Edward SimbeyUPDATES.!
LISSU: Mheshimiwa Hakimu katika hoja za upande wa Jamhuri wakiomba nisipewe dhamana wametoa refference ya kesi za Afrika Kusini. Lakini wamesahau kuwa sheria hizo ni za mwaka 1976 ambapo kilikuwa ni kipindi cha Ubaguzi wa rangi. Kwahiyo sheria hizo haziendani kabisa na kwetu. Huwezi kutumia sheria zilizotungwa kipindi cha ubaguzi kama rejea katika nchi isiyo na ubaguzi. Kwahiyo Mheshimiwa Hakimu naomba upuuze hoja hiyo ya upande wa Jamhuri.
HAKIMU: Mhe.Lissu endelea......
LISSU: Mheshimiwa Hakimu kwa sheria za Tanzania zimeeleza kwa kina sababu za kumnyima mshtakiwa dhamana. Na katika sheria hizo hakuna mahali imeelezwa kwamba kufanya makosa mahali pamoja ni kigezo cha kunyimwa dhamana. Jamhuri haiwezi kuzuia nisipewe dhamana kwa sababu ya unprove allegations..
Mheshimiwa Hakimu pia maombi yaliyowasilishwa na Jamhuri ya kuzuia dhamana kwangu yamekuja kwa kiapo bila kuwa na Application hivyo ni batili. Mheshimiwa kiapo hiki hakina application, kipo kwenye upepo, kwahiyo kitupiliwe mbali...
HAKIMU: Mhe.Lissu endelea...
LISSU: Mheshimiwa kuna hoja ya judicial notes na kwa yote hakuna kifungu chochote kinacho nizuia kupewa dhamana na huwezi kuchukua judicial note kwa hoja ya judicial progressive. Hoja ya kuninyima dhamana uikatae maana hakuna kifungu chochote kinachokataza dhamana hii. Kwa mujibu wa kifungu cha 148 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai dhamana yangu ipo wazi.
HAKIMU: Upande wa Jamhuri mna cha kusema?
JAMHURI: Mheshimiwa Hakimu tunaomba kiapo kilichopokelewa Mahakamani kitumike na ndio ushahidi wetu hivyo tunaomba dhamana ifungiwe.
HAKIMU: Kwa sheria ipi?
JAMHURI: Kwa ile sheria ya Afrika Kusini. Hata kama ilitungwa kipindi cha ubaguzi lakini bado haijabatilishwa. Kuhusu uhalali wa kiapo chetu kukosa application Mheshimiwa sio lazima application iwe writter formal, hata oral inaruhusiwa.
HAKIMU: Mbona sikuelewi!! sasa ile afidavity (hati ya kiapo) mlioniletea niiweke kama chamber samansi au Oral?? (Ukumbi mzima umecheka).
JAMHURI: Mheshimiwa Hakimu kwa kumalizia naomba Mahakama itupilie mbali maombi ya mshitakiwa na ikubali maombi ya Serikali.
HAKIMU: Natoa maamuzi hapa hapa nipeni kitabu changu.
(Hakimu anapewa kitabu)........
Kwa hisani ya Edward Simbey
HAKIMU: Upande wa Jamhuri umewasilisha kiapo cha kamishina na umeeleza sababu za kutotoa dhamana kwa mshtakiwa. Kimsingi kutokana na Personal knowledge ambayo wakili wa jamhuri ameipata katika chanzo chake anasema mtuhumiwa atarudia kosa tena ikiwa atapewa dhamana. Mahakama hii imeombwa kuweka zuio la dhamana. Upande wa Jamuhuri umetoa baadhi ya vifungu vya sheria ya Afrika Kusini viwe cited ktk kesi hii. Vilevile kuna Mwandishi wa sheria amekuwa cited katika kuzuia dhamana hii......
Anasimama kdg kisha anaendelea....
HAKIMU: Katika majibu yake mshitakiwa amekishambulia kiapo kilichowasilishwa na upande wa Jamhuri. Amesema kiapo hicho hakina viwango vya viapo kutoka kwa kamishna wa viapo. Kwamujibu wa mshitakiwa kiapo hicho hakina Tarehe wala anuani. Mshitakiwa anaongeza kwamba muhuri wa Wakili kamwe hauwezi kuwa mbadala wa anuani. Mshitakiwa aliendelea kusubmit kwamba hawezi kunyimwa dhamana kwa sheria hizo zilizotajwa. Mshitakiwa aliieleza Mahakama kuwa sheria za Afrika kusini (zilizotungwa kipindi cha ubaguzi) haziwezi kuwa applied Tanzania. Mshitakiwa pia alishangazwa kama Mahakama hii inaweza kumnyima dhamana kwa kuwa hata watoa mashitaka hawajatoa vifungu vya sheria.
Anaendelea.....
HAKIMU: Mshitakiwa ameshangaa pia kama Mahakama inaweza kumnyima dhamana ambayo ni haki yake ya msingi kikatiba. Mshitakiwa ameomba pingamizi hilo la dhamana litupiliwe mbali.
Upande wa jamuhuri umeeleza kuwa kiapo chao kina anuani na sahihi ya kamishina. Upande wa Jamhuri umeongeza kuwa mshitakiwa asijaribu kuishawishi Mahakama kwa namna yoyote ile, pia umekazia kuwa lazima Mahakama ifanye citation kwenye vitabu vya mwandishi wa sheria waliyemtaja. Pia Jamhuri imesema kuwa sheria ya Tanzania peke sio msahafu katika maamuzi. Kadushi (Wakili wa serilali) alimshangaa mshitakiwa kuwepo samansi chamber..
Baada ya kusikiliza pande zote mbili sasa ni zamu yangu......
HAKIMU: Maoni yangu ni kwamba huwa tunalazimika kukopa sheria kwa maneno ambayo ni ambiguous. Kifungu cha 148 kifungu kidogo cha 5 kinatoa orodha ndefu ya watu wasio pewa dhamana. Jamuhuri hamkujiaelekeza ndani ya kifungu hicho kama kipo kipengele kinachozuia dhamana. As much as a citations mlizoleta hapa Mahakamani.
HAKIMU: Nikimnyima Mtuhumiwa dhsmana kwa hoja hizo nitafanya Mahakama iamini tuhuma dhidi ya mtuhumiwa bila kuwepo kwa ushahidi wa kisheria. Na Mahakama hawezi kufanyia kazi tuhuma ambazo hazijathibitishwa. Kwa mazingira ya sheria zetu hao Waandishi ambao Upande wa Jamhuri umewacite ktk vifungu vyao haviwezi kuwa applicable ktk mahakama hii. Na hao Waandishi hawajawahi kutuonesha vifungu vyao juu ya kuzuia dhamana.
HAKIMU: Ni kweli kwamba Mshitakiwa anaweza kunyimwa dhamana lakini kwa Statuts zinazoeleweka. Kiapo kilicholetwa na Jamhuri kina shorts standard nyingi na hakiwezi kuwa kiapo halali. Hakina Tarehe na wala hakioneshi anuani. Haishangazi MTU kwenda kumuaproach Kamishna wa viapo huku ukiwa umesaini kila kitu. Ndio maana sheria inataka kamishna aoneshe Tarehe, mahali na siku.
Hivyo basi natupilia mbali zuio la dhamana lilowekwa na Upande wa Jamhuri na ninatoa ruhusa kwa mshitakiwa kujidhamini mwenyewe kuwa hundi ya shilingi Milioni 10."
Hakimu anagonga meza.. amemaliza kusoma rulling. Mawakili wa Serikali wamesimama. Wanapinga maamuzi ya Hakimu.
HAKIMU: Upande wa Jamhuri mnasemaje?
JAMHURI: Mheshimiwa Hakimu tunatoa ombi la kukata rufaa kwa mujibu wa kifungu cha 376 kifungu cha kwanza cha CPA.
HAKIMU: (huku akiandika) Enhe endelea....
JAMHURI: Mheshimiwa tunayo hoja ya kisheria ya kupinga maamuzi haya. Kimsingi hoja yetu ni kwamba kwakuwa tayari tumeshaomba kukata rufaa upande wa Jamuhuri tunaomba tuwasilishe kwa kifungu cha 133.
Hakimu anasoma kifungu husika, kisha anampa Lissu muda wa kujibu hoja. Upande wa Jamhuri unapinga.
HAKIMU: Hivi upande wa Jamuhuri unataka tutumie kifungu gani cha mimi kutoa maamuzi katika hoja mliyoikatia rufaa!?? Mimi nimeshamtoa maamuzi kuwa mshitakiwa ajidhamini kwa hundi ya Shilingi milioni 10. Kama Jamuhuri mna hoja nyingine, subirini mahakama hii iahirishwe kisha mkamateni upya. Lakini hamuwezi kunilazimisha kufanya maamuzi nje ya Sheria.
Mawakili wa serikali wanalalamika......
HAKIMU: Mimi tayari nimeshaamua na mpaka sasa hakuna Mahakama iliyotengua uamuzi wangu, hivyo kama mnataka kuvunja huo uamuzi wangu fanyeni. Karani panga Tarehe nyingine ya shauri. The court is dismissed.!
#MyTake:
Let the Glory be to GOD. Asante Kamanda Edward Simbey kutoka chumba cha Mahakama Kisutu kwa updates hizi. Binafsi namuombea baraka nyingi Hakimu aliyesikiliza kesi hii. Amedhihirisha weledi wake ktk taaluma ya sheria. Huu ni ushindi wa kwanza wa HAKI dhidi ya UONEVU na Udikteta uchwara.!
Let the Glory be to GOD. Asante Kamanda Edward Simbey kutoka chumba cha Mahakama Kisutu kwa updates hizi. Binafsi namuombea baraka nyingi Hakimu aliyesikiliza kesi hii. Amedhihirisha weledi wake ktk taaluma ya sheria. Huu ni ushindi wa kwanza wa HAKI dhidi ya UONEVU na Udikteta uchwara.!
0 comments:
Post a Comment