Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani.
Upungufu huo unaowapa wadukuzi mlango wa nyuma wa kuiga herufi za siri uligunduliwa baada ya watafiti wa hali ya ubora wa programu Checkpoint walipojaribu kusuluhisha hitilafu iliyowezesha kirusi kuambukiza makumi ya mamilioni ya simu zilizokuwa na programu zilizoundwa na kampuni moja ya Marekani Qualcomm.
Kampuni hiyo inayounda programu za simu imeuza programu hiyo kwa watengenezaji wa simu milioni 900.
Hilo linamaanisha kuwa simu milioni 900 zipokatika hatari kubwa ya kudhibitiwa na wadukuzi.bbc
0 comments:
Post a Comment