Watabiri wa hali ya hewa wanasema Kimbunga Nicole kinaendelea kuimarika huku kikielekea kukaribia kisiwa cha Bermuda katika bahari ya Atlantiki.
Kimbunga hicho kimesababisha tufani ambayo imefikia kiwango cha daraja la tatu.
Kimbunga hicho kina upepo unaosafiri kwa kasi ya zaidi ya kilomita 200 kwa saa.
Inakadiriwa kwamba kimbunga Nicole kitafikia eneo hilo ambalo linamilikiwa na Uingereza baadaye Alhamisi.
Maafisa wa serikali wamewahimiza watu kusalia manyumbani.
Wiki iliyopita, kimbunga kingine kwa jina Matthew kilipiga maeneo ya Haiti na kuua mamia ya watu.
Mafuriko yaliyotokana na kimbunga Matthew pia yalisababisha uharibifu Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Jamaica na majimbo ya Florida na Carolina Kaskazini nchini Marekani. BBC
0 comments:
Post a Comment