Muimbaji Janet Jackson amethibitisha rasmi kwamba anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50.
Ameliambia jarida la People: "Tunashukuru Mungu kwa baraka tuliyonayo", na akapigwa picha na tumbo lake linalozidi kuwa kubwa kudhihirisha uja uzito.
Fununu kuhusu uja uzito wake zilizuka Aprili alipojitokeza kuahirisha shughuli zake na tamasha la kimataifa 'Unbreakable' akisema anataka kupanga uzazi na mumewe Wissam al-Mana.
Ameonekana hivi karibuni London akinunua vitu katika duka la watoto.
Jarida la The People limenukuu duru iliyo karibu na familia ya Jackson aliyesema: "Ana furaha sana kuhusu uja uzito wake na anedelea vizuri sana. Ana raha kuhusu kila kitu."
Katika video iliowekwa kwenye Twitter mwezi April, amewaambia mashabiki wake kuwa ana ahirisha shughuli zake, kwasababu "kumekuwa na mabadiliko ya ghafla".
"Nilidhani ni muhimu mujue kwanza. Mimi na mumewangu tunapanga familia yetu," alisema, na kuongeza: "Tafadhali iwapo munaweza, jaribu muelewa kuwa ni muhimu nifanye hivi kwa sasa."
Aliendelea kusema: "Ni lazima nipumzike, ni agizo la daktari."
Janet Jackson ni nani:
- Janet Damita Jo Jackson alizaliwa Mei 16 1966 Gary, Indiana Marekani
- Ni mdogo katika ndugu tisa na ni dadake muimbaji nyota Michael Jackson
- Alitoa albamu yake ya kwanza Janet Jackson mnamo 1982
- Ana albamu 11 ya hivi karibuni ikiwa ni Unbreakable, iliotolewa 2015
- Ni mshindi mara 7 wa tuzo ya Grammy
- Alianza taaluma yake kwa kushiriki katika kipindi cha televisheni The Jacksons mnamo 1976 na ameshiriki katika filamu kadhaa ikiwemo ya Tyler Perry 'Why Did I Get Married'
- Muimbaji huyu ameolewa na mumewe wa tatu, Bilionea raia wa Qatari Wissam al-Mana, 2012.
Janet Jackson sio mwanamke maarufu wa kipekee kuzaa katika umri mkubwa.
Mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry amezaa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47, miaka mitatu iliyopita.
Mkewe John Travolta, Kelly Preston amezaa mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.bbc
0 comments:
Post a Comment