Mamia ya watu wamekusanyika eneo la Freedom Corner katika Uwanja wa Uhuru Park, katikati mwa jiji la Nairobi, kuandamana kulalamikia wanachosema ni ongezeko la visa vya ufisadi serikalini. Maandamano hayo yanafanyika siku chache baada ya gazeti moja kuchapisha habari zinazodai jumla ya dola 50 milioni za Marekani katika wizara ya afya zilitumiwa vibaya au zikaporwa.
Serikali imekanusha madai hayo.
Wanaharakati walioandaa maandamano ya leo wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta achukue hatua la sivyo ajiuzulu.
Polisi wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.
0 comments:
Post a Comment