mwanazuoni

MOFIMU NA AINA ZAKE


Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Katia mada hii utaweza kujua vipashio vya msingi vinavyohusika katika mchakato wa uundaji wa maneo. Pia utajifunza michakato mbalimbali inayohusika katika uundaji wa maneno na dhima zake.
Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya.  Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano.  Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiliamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.
MOFIMU
Fasili ya mofimu ni: Mofimu ni neno au sehemu ya neno yenye maana kisarufi, ambayo haiwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana. Kwa mfano:
maneno
(a) babu, hewa
mofimu         
  • kila neno lina Mofimu moja
AINA ZA MOFIMU
  1. Mofimu huru
  2. Mofimu tegemezi
MOFIMU HURU
Haya ni maneno kamili ambayo huwezi kugawa zaidi bila kupoteza maana.
Mfano
Baridi, kofia, hewa, kaka, mama, sana, maji. Maneno haya hayawezi kugawanyika zaidi na yakaendelea kuwa na maana hiyohiyo kisarufi.
MOFIMU TEGEMEZI
Ni vipande vidogovidogo vya maneno vyenye maana kisarufi. Mofimu hii maneno yamejengwa kwa kubandika vipashio kadhaa vya  kisarufi ambavyo huweza kubadilishwa  na maana ya neno ikabadilika.
Mfano
Neno anapika lina mfano tegemezi ufuatazo:-
-a  -na-     -pik-     -a; lina mofimu tegemezi tatu
 1   2        kiini      3
Dhima na maana ya Mofimu hizo ni:-
a- inaonyesha idadi yaani umoja vile vile huonyesha nafsi ya tatu umoja (3).
-na- inaonyesha wakati uliopo (njeo iliyopo)
-pik- kiini cha neno.
-a irabu ya mwisho ya kitenzi
Mofimu tegemezi haziwezi kusimama peke yake kama ilivyo Mofimu huru. Ni lazima zipachikwe katika mzizi wa neno au kiini cha neno ambayo ni sehemu ya neno iliyobeba maana ya msingi ya neno hilo.  Mzizi/kiini hakibadiliki.
Hebu chunguza mifano zaidi ya Mofimu tegemezi katika jedwali hapo chini.
NENO
MOFIMU
MZIZI/KIINI
MOFIMU TEGEMEZI
Anacheza
a-na
-cheza
-a
Walicheza
Wa-li
-cheza
-a
Atacheza
a-ta
-cheza
-a
Tumecheza
Tu-me
-chez
-a
Aliyecheza
a-li-ye
-chez
-a
DHIMA ZA MOFIMU
Uundaji wa maneno kwa kutumia Mofimu, hutegemea kiini kimoja cha neno kuweza kuzalisha msamiati mwingi.  Maneno hayo hupatikana kwa kubadili Mofimu.
Mofimu hizo zina kazi (dhima) tofauti za kisarufi kutegemea matumizi ya neno.
  1. Mofimu huweza kutokeza nafsi, mtenda na idadi.
    Mfano
  • Ninalima  ) inaonyesha Mofimu nafasi ya kwanza umoja wa mtenda jambo.
  • Tunalima ) inaonyesha Mofimu ya kwanza wingi.
  • Unalima   ) inaonyesha Mofimu ya mtenda nafsi ya pili umoja.
  • Mnalima  ) inaonyesha Mofimu ya mtenda nafsi ya pili umoja.
  • Analima   ) inaonyesha Mofimu ya mtenda nafsi ya tatu umoja.
  • Wanalima) inaonyesha Mofimu ya mtenda nafsi ya tatu umoja.
2. Mofimu hutambulisha njia au wakati.
  • A-na-cheza; -na-, inanyesha Mofimu njeo iliopo.
  • A-ta-cheza; -ta-, inaonyesha Mofimu njeo ijayo.
  • A-me-cheza; -me- inaonyesha Mofimu njeo timilifu
3. Mofimu huonyesha umoja na wingi wa nomina na viwakilishi.
  • Kisu;  ki- inaonyesha umoja
  • Visu; vi- inaonyesha  wingi
  • Msafi; m-, inaonyesha umoja
  • Wasafi; w-, inaonyesha wingi
  • Kidonda; ki-, inaonyesha umoja
  • Vidonda; v-, inaonyesha wingi
4. Mofimu hutambulisha urejeshi wa mtendaji/mtenda au mtendewa.
Mfano:
  • A-na-ye-sema; -ye-, ni Mofimu ya urejeshi wa mtenda
  • A-na-m-penda; -m-, ni Mofimu ya urejeshi wa mtendewa
  • a-li-ni-himiza; -ni-, ni Mofimu ya urejeshi wa mtendewa
  • ki-li-cho-vunjika; -cho-, ni Mofimu ya urejeshi wa kitu

5. Mofimu huonyesha uyakinifu na ukamilisha (yaani kukubalika au kukataliwa au kutofanyika kwa jambo.
Mfano:
YAKINISHI                                       UKANUSHI
  • Anaimba                                     Hataimba
  • Alicheza                                      Hakucheza
  • Ninaimba                                     Siimbi
6. Mofimu za kutendesha au kusababisha Mofimu hii inaonyesha hali ya kutendesha au kusababisha jambo fulani.
Mfano:
  1. Amemaliza
  2. Amemlisha
  3. Amechezesha
7. Mofimu ya kusifia na kudunisha.
Kusifia               Kudunisha
  • Mtoto             Kitoto
  • Mzee             Kizee
  • Nyumbu         Kijumbu
  • Jito                Kijito
8. Mofimu zinazoonyesha hali za vitenzi
Hali ya kutendewa
  • Anasomewa
  • Mtahiniwa
  • Anachezewa
Hali ya kutendeana jambo
  • Wanapigana
  • Wanapendana
  • Wanasomeana
Hali ya kutendea
  • Alimlimia
  • Alimchezea
  • Nilimpikia

UAMBISHAJI WA MANENO
Uambisha wa maneno kitendo cha kupata kwa kubandika Mofimu  kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig-unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga mpigaji, amepigika nk.
Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.
Katika lugha ya Kiswahili  viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.
Mfano
Wanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.
Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.
Angalia mifano ifuatayo
Neno
Viambisha Awali
Kiini
Viambisha Tamati
Unapendelea
u-na-
-penda-
el-e-a
Waliongozana
wa-li-
-ongoz-
an-a
Analima
a-na-
-lim-
-a
anayeiimbisha
a-na-ye
-imb-
-ish-a
DHIMA ZA UAMBISHAJI
  1. Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa  kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake uleule.
Mfano
Fundisha kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini  kilichocho kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.
  1. Uambishaji huonyesha nafsi
  2. Uambashaji huonyesha njia (muda)
  3. Uambishaji huonyesha urejeshi
  4. Uambishaji huonyesha ukanushi
  5. Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi
Vitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomini.
Mfano
Vitenzi                      Kiini               Nomino                                 Vitenzi
Cheza                         -chez-             Mchezaji, mchezo                  wanacheza/atamchezea
Piga                              -pi-               Mpigaji,Mpiganaji                    watanipiga, aliyempiga/wanaompiga
Uambisaji hutumika kuzalisha  viwakilishi na vielezi.
Neno (kiwakilishi)                        Kiini               Kielezi
                        Huyu  Huyo                                    Hu                   Humu humo
                       Wangu, wako, wake                         wa
                       Hii, hizo, hiki                                     Hi
Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.
Mfano
Neno: Hawakulima
  • Ha-, kiambishi cha ukanushi
  • Ku-, kiambishi njeo/wakati
Viambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.
Dhima
Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho usababishi.




Neno
Viambishi Tamati
Anapiga
-a
 Wanapigana
-an
Asipigwe
-w
Amempigisha
-ish-

Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa
Kutokea  na vitenzi.
Neno
Kiini
Viambishi Tamati
Piga
pig-
-o
Mchezo
chez-
-o
Mtembezi
tembe-
-z-i
Mfiwa
-fi-
-us-a
Onyesha katika maneno yafuatayo:-
MNYUMBULISHO
Mnyumbulisho ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta kuongeza urefu wa kitu hicho.
Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulish katika katika kiini ili kupata msamiati mpya.  Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.
Viambishi vinapochukuliwa katika kiini  cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno  mengine mpya, kama lim-ishwa, kim-iki-a, lim-ia, lim-w-a.
Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina kwa mfano.
Neno
Kiini
Shina
Maneno ya Mnyumbuliko
Elekea
elek
eleka
Elekeana, elekea, elekwa, elekesha
Shikishana
shik
shikisha
Shikishana, shikisha, shikishaneni
Kwa ujumla tunawaza kusema kwua maneno ya kawaida hunyumbulika.  Hivyo kiina/mzizi au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatoka na msingi mmoja wa maana.


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. Asante kwa somo na mada nzuri naomba uendelee kuweka mada za elimu

    ReplyDelete