![]() |
Suruali ya ndani ya mkewe Adolf Hitler imepigwa mnada |
Nguo ya ndani ya mke wa Adolf Hitler Eva Braun imeuzwa katika mnada kwa pauni 3000.
Suruali
hiyo ikiwa ni miongoni mwa vitu vyengine vya bi. Braun ilipigwa mnada
katika jumba la mnada la Phillip Serrell huko Melvern ,ikitarajiwa
kuvutia pauni 400 lakini ikauzwa kwa pauni 2,900.Pete ya dhahabu na kiboksi chenye kioo kilichokuwa na lipstiki nyekundu ya Eva Braun pia kiliuzwa.Vyote hivyo viliuzwa kwa mtu binafsi.
Pete ya dhahabu iliozungukwa na madini iliuzwa kwa pauni 1,250 huku lipstiki hiyo ya rangi ya fedha ikiuzwa kwa pauni 360.
Wakati huohuo picha za rangi nyeupe na nyeusi za Eva Braun na Adolf Hitler ziliuzwa kwa pauni 100.
0 comments:
Post a Comment