Na: Mwandishi Wetu.
Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuwajali wanyonge hasa katika mambo yanayohusu elimu.
Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Shirikisho hilo Zenda Daniel wakati wa mkutano wao na waandishi wahabari kuhusu mambo sintofahamu ya juu ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.
Zenda alisema kuwa wao kama Shirikisho wanampongeza na kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuwakwamu wanyonge
“Sisi kama Shirikisho tunampongeza na kumuunga mkono mweshimiwa Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha wanyonge wanajikwamua kwakupata elimu bora”. Alisema Zenda.
Pamoja na pongezi hizo Shirikisho hilo limeelezea masikitiko yake kwa kile kinachoendelea kuhusiana na suala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hadi kufikia hatua ya kultilia shaka uwepo wa baadhi ya watendaji wa Serikali kufanya hujuma ili kukwamisha azma ya Serikali kutoka mikopo kwa wate wanaostahili.
Katika duku duku lao walionyesha miongozo miwili tofauti kuhusiana na vigezo vya wanaostahili kupewa mikopo, mmoja ukitolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku mwingine ukitolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo walisema vigezo vilivyiwekwa kwenye miongozo hiyo vinakinzana.
Zenda aliongeza kuwa hata pale wanaposema kigezo cha watoto uyatima kinapopaswa kutumika kumekuwa na changamoto kwani kuna baadhi ya wanachuo ambao wamethibitika kuwa ni yatima lakini hawajapewa mkopo hadi sasa.
Aidha walitumia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa Serikali kupitia Wizara husika kukaa pamoja na Bodi ya Mikopo ili kupitia upya vigezo vinavyotumika kuwapata wanafunzi wanaostahili mikopo hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa Hamasa wa Shirikisho hilo Nganwa Nzota alitoa angalizo kwa Bodi ya Mikopo kwa hatua yake ya uhakiki ambapo imelenga kuwaondoa wale wote watakao kuwa hawana sifa kulingana na vigezo vya sasa kuwa italeta mkanganyiko mkubwa utakasababisha watu waichukie Serikali yao.
Alishauri kuwa zoezi la uhakiki liendelee lakini lisihusishe kuwaondolea mikopo wanufaika hao watakaobainika kutokidhi vigezo vya sasa kwani wao tayari wana mikataba nao na badala yake wajikite kuhakikisha wanakuwa makini kwa waombaji wapya.
Katika Mkutano huo maalum uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bwana Hamid S. Muhina Sherikisho hilo liliiomb Serikali ya Rais Dkt. Jonh Pombe Magufuli kupitia upya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu hili kuongeza ufanisi wake.(P.T)
0 comments:
Post a Comment