Mbunge Wa Jimbo la Masasi. Dr Rashid Chuachua
Ametoa taarifa kwa wananchi wake kupitia ukurasa wake Wa Facebook wenye ujumbe huyu. " Habari Za mda huu Wapendwa wanamasasi. Kuna taarifa mbili zinazotatiza na zinatafutiwa ufumbuzi.
1. Ni kuadimika Kwa siment na kupanda bei ghafla. Kuhusu hili nimeshaongea na waziri WA viwanda na biashara mhe. Mwijage na amenijibu anafanya mawasiliano na Dangote atanipa majibu yanayoeleweka kuhusu sakata hili. Majibu hayo nitayaleta kwenu. Poleni Sana Kwa kadhia hii.
2. Ni kukamatwa kamatwa Kwa wananchi wanaobeba mkaa. Tayari nimeongea na mamlaka ya juu ya wilaya na ninasubiri Maelezo nayo nitayaleta kwenu. Nina kiu ya kuona wananchi wanaishi bila kero. Mungu awabariki Sana."
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment