mwanazuoni

KILIO CHA WANYONGE WA KAWE KUHUSU DIWANI CUP 2016



TAMKO LA KILIO CHA WANYONGE WA KAWE KUHUSU DIWANI CUP 2016

Kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuweza unipa siha njema na kuweza kunipa uwezo wa kushika kalamu na karatasi kuandika andiko ili la KILIO CHA WANGONGE WA KAWE KUHUSU DIWANI CUP 2016.
Pia nifaraja kwangu kuona katiba ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 18(a) – (e) inanipa uhuru kwa kufanya jambo hili. Asante Tanzania.
Kabla ya kwenda kwenye nukta ambazo nimepanga kuzijadili japo kwa upana wake, napenda kuanza kwa kuangalia maana ya uongozi na kiongozi. Maana ya Uongozi.
Uongozi ni dhana, taaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaongozwa kuunganisha nguvu, stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao.
Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaongozwa na njia ya kufikia lengo lao.
Tunaweza kuwagawa viongozi katika mafungu yafuatayo kulingana na jinsi walivyoingia madarakani na namna wanavyoongoza kama ifuatavyo:
a.      Wale wanaopata uongozi kwa kurithi.
b.     Wanaopata uongozi kwa kuchaguliwa na watu
c.     Wanaojitwalia mamlaka ya kuongoza.
d.     Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.
Uongozi wa Kidemokrasia ni upi?
Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha watu katika kufanya maamuzi na utekelezaji wake.
Sifa za Kiongozi bora.
Kuna sifa nyingi za kiongozi bora ikiwa pamoja na maadili, uaminifu, ufahamu n.k lakini mimi najikita katika Maadili.
Maadili : kiongozi ni lazima akubarike katika jamii anayoiongoza. Ili akubarike ana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi zake. Kiongozi mwongo, mlevi,mvivu, asiye mwaminifu n.k hawezi kuwa kiongozi.
Baada ya kuangalia za dhana nzima ya uongozi japo kwa uchache. Ni muda wa kujadili kilio cha wanyonge kuhusu Diwani Cup Kawe 2016. Nitajikita kwenye nukta kadhaa ambazo ni msingi wa andiko languhili la wanyonge wa Kawe.
Ø Je tunamalengo ya kuleta Maendeleo KAWE ?
Ø Je kazi ya Kiongozi kushirikisha na kuunganisha nguvu kwa wananchi wake inafanyika ?
Ø Mashindano ya Diwani Cup Kawe yalikuwa na dhamira ipi?
Kabla niseme sitozungumzia kiingilio wala zawadi ina thamani gani? Nitazungumzia wananchi wa KAWE wamepata athari zipi?. Kuna athari mbali mbali zimepatikana kutokana na Mashindano ya DIWANI CUP KAWE kuwa na Sura ya Kihuni. Jambo ambalo wapenda Maendeleo tunapinga kwa nguvu zote. Athari tulizopata wanyonge wa Kawe na Wapenda Maendeleo ni kama ifuatvyo:
       i.            Kutugawa wanaKawe kwenye makundi mawili au zaidi.
Baada ya mashindano haya kuisha katika sura ambayo imeleta mkanganyiko umepelekea kutufanya sasa wanajamii kuwa na makundi mawili au zaidi. Hali ambayo katika ustawi wa maendeleo ni hatari kubwa sana. Leo kuna watu  kawe walikuwa marafiki awezi kuombana hata maji lakini haya yamefanywa na wale ambao tumewapa dhamana ya kutuongoza tena kwa njia ya kidemokrasia. Naanza kupata mashaka na kura yangu  pia inanipa mashaka tena katika kuchagua viongozi kipindi kijacho. Kawe tunaitaji umoja wetu uendelee lakini kwa kupitia Mashindano ya Diwani Cup Kawe mmevunja Umoja wetu hii ni athari kubwa iliyofanywa na watu wachache bila ya kuangalia maslahi ya umma na kuweka maslahi yao binafsi mbele.

      ii.            Kuharibu taswira na heshima ya Kawe kwenye Uga wa Michezo.
Kawe ni miongoni mwa maeneo yaliyojijengea sifa kubwa katika wilaya ya kinondoni hasa kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Nakumbuka kipindi kile bado nipo shule ya msingi tulipokuwa tunakwenda msasani kwa miguu kuangalia timu za kawe zilipokuwa zinacheza na kwa kweli Msasani Palikuwa panajaa endapo timu za kawe zikicheza. Timu ambazo ziliipa sifa kubwa kawe kwa kipindi kile ni Ukwamani, Kawe Ranger na Maskani Fresh. Mimi nilikuwa maskani fresh sikumbuki kwa nini nilitokea kuipenda maskani fresh labda kwa kuwa walikuwa wanawachezaji wazuri. Nakumbuka ila leo KIFA tumepeleka sifa mbaya sio sifa zile za mwanzo leo Kawe inaonekana kuna viongozi wapiga dili ‘ matapeli’. Una hoja za msingi za kuvunja mashindano kwa kufata sheria zako za mashindano kwa nini ukimbie wito wa KIFA? Mimi najiuliza tu.

  iii.            Kuwanyima burudani Wanakawe
Huku ni kuwanyima burudani wana Kawe. Kitendo hiki akikupaswa kufanywa au ndani yake kuwa na kiongozi alipewa mamlaka ya kuwaongoza wananchi. Nakumbusha tu ….
kidogo Uongozi ni dhana, taaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaongozwa kuunganisha nguvu, stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao.
Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaongozwa na njia ya kufikia lengo lao

Lengo la wana Kawe ni burudani hasa kupitia mpira wa Miguu lakini kiongozi unakuwa katika kushiriki kuharibu burudani je unajua lengo la Uongozi? Hapa Mshana Nauliza tu kwa nia ya kujenga.
Kwa uelewa wangu wa majukumu ya KIFA na Nguvu walizokuwa nazo za kisheria na kimamlaka wana Uwezo wa kufungia mashindano kutofanyika KATA ya Kawe. Je wakifanya hivyo sisi tuende wapi? Leo Mshana nikashuhudie mpira Kunduchi? Ninafaidika na nini kwa serikali kutuachia kiwanja? Nifahamiana vipi na ndugu zangu wa mzimuni tukiwa pamoja. Moja ya lengo la Mashindano yoyote yale duniani ni kuleta umoja na mshikamano. Viongozi mnalakujibu juu ya dhuruma mnayotufanyia wanyonge wa kawe.



   iv.            Kuua vipaji vya wana Kawe Wanyonge
Lengo lilikuwa lipi la kuanzisha mshindano la DIWANI CUP KAWE 2016?
Mtanisaidia waandaaji wa diwani cup . Hivi kwa mwenendo mbovu huu tunaweza kweli kukuza vipaji au atujui thamani ya vipaji? Tunaua vipaji kwa gharama nafuu kwa kuweka maslahi binafsi mbele.
Hizi ni athari na kilio cha Wanyonge wa Kawe Kuhusu Diwani Cup.
Kwa nini haya yametokea? Je yametokea kwa Bahati mbaya au yamepangwa? Nasema haya yametokea kwa malengo maalumu ya Watu Fulani. Ithibati za kusema hivyo ninayo ila najielekea kwenye sababu zifuatazo:
Sababu hizi zinaonyesha na zinatufanya WANYONGE WA KAWE TULIE, hizi sababu zimepangwa kwa kupitia maeneo haya kama ifuatavyo:
·        Viongozi kuwa viashiria vya ukosefu wa maadili.
Waliokuwa wanaendesha mashindano haya wanaonekana wazi kuwa wana viashiria vya ukosefu wa maadili. Kwa nini nasema yawezekana wana viashiri vya ukosefu wa maadili kwanza nikumbushe tena kidogo …. Maadili : kiongozi ni lazima akubarike katika jamii anayoiongoza. Ili akubarike ana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi zake. Kiongozi mwongo, mlevi,mvivu, asiye mwaminifu n.k hawezi kuwa kiongozi. Unakaa na viongozi wa timu Fulani mathalani Kawe Veterani na kukubaliana nao wasilipe kiingilio halafu kesho unawaambia walipe ? una maadili ya uongozi kiongozi apaswi kuwa mwongo. Lakini anatokea mtu anajitolea kuendeleza vipaji kwa kujitolea mipira kwa timu iliyoshinda wewe uankwenda nayo kwako na watu wanapofata unaleta uswahili tena mbele ya mgeni unajenga taswira gani ? na kiongozi wenye mamlaka ya kuwatumia wananchi unashindwa kukemea , maadili yako ya uongozi yapo wapi? Kwa maana hiyo yaliyotokea yamepangwa na kubarikiwa na uongozi.
·        Zawadi ya mshindi kutolewa nyumbani kwa mwanzilishi wa mashindano.
Sijawahi kusikia wala kuona sehemu nyingine duniani ispo kuwa Kawe Yetu. Leo nilikuwa napitia nyaraka mbalimbali na kupitia documentary za waanzishi wa mashindano ya mpira wa miguu na mashindano mengine duniani nimeshindwa kupata kuona zawadi ikitolewa kwa mtindo huu. Kwa ambaye amewai kuona au kusikia nje ya Kawe naomba anitumie kupitia email yangu halfanm8@gmail.com kama ana video anitumie whatsapp kwa namba hii 0712474810. Nina kila sababu ya kusema kuwa yaliyotea yana Baraka zote za Uongozi na yalipangwa.

Nina mengi ya kusema Mnyonge mimi na wezangu Poleni Wanyonge Wezangu Tufute machozi na tumlilie Mungu kwa Kusema Yana Mwisho Haya Yote kwa Uwezo wake. YATATIMIA


MSHANA B. HALFAN
MSEMAJI WA WANYONGE WA KAWE
06.12.2016
MASASI.


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment