mwanazuoni

MBUNGE WA JIMBO LA MASASI DR RASHID CHUACHUA AFANYA ZIARA CHISEGU

Pia Nilitembelea mtaa wa Chisegu leo tar 16/12/2016 nilikwenda gharani kuona namna na taratibu za ukusanyaji wa korosho na kujionea changamoto zake nimeagiza kuwatangazia Wananchi wote kwa ujumla kuwa wapeleke Korosho haraka ili kuwahi minada miwili itakayofanyika kabla ya krismas na naomba kila atakayesoma hamualifu na wenzie maana tunaelekea mwishoni mwa msimu na minada inaonesha Kushuka kwa bei.
Pia kuhusu malipo tumemwaagiza mkuu wa wilaya kuhakikisha ana simamia malipo yote kwa wakati na ametuahidi hadi kufika tar 31/12/2016 malipo yote yatakuwa yamekwishafanyika.
Pia nilitembelea Mradi wa ujenzi waofisi ya Mtaa wa Chisegu na mradi wa ofisi ya mtaa wa Tuleane ambao wako kwenye hatua mzuri wote.
Vilevile nilofanya mkutano wa hadhara na kupokea changamoto na ushauri wao kuhusu jimbo letu, nimewaaeleza adhima ya ofisi ya mbunge kwanzia mwezi wa 12 huu tunaanza ujenzi wa Wodi na chumba kujifungulia mradi huu ni kutoka ofisi ya mbunge kama ilivyo adhima yangu ya kuwa na vituo vitatu vya afya katika jimbo la Masasi. Nimemwaagiza Mtendaji wa kata ikifika Juma Tatu wanieletee gharama na ramani ya majengo hayo kama nilivyokaagiza kupitia ofisi yangu na ameniambia vipo tayari juma Tatu atanikabidhi.
Pia nilipata taarifa za hali mbaya ya utupaji wa taka katika Damp la Chisegu, niliamua kwenda na kujionea ni kweli taka hazitupwi katika eneo husika wengi wao wanatupia barabarani, mwezi wa 4 nilipata malalamiko hayo nikamwaagiza Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji na Bwana afya kufuatilia hili lakini leo yanarudia haya haya, Wahusika wa kutupa taka wanajulikana naomba wajirekebishe kabla hatuna wahuni pia hatua za kisheria.
Tujitolee kuleta maendeleo Masasi ni mimi, wewe na yule...
 Mbunge wa Jimbo la Masasi Dr Rashid Chuachua akisisitiza jambo fulani katika mradi.




 
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment