mwanazuoni

SERIKALI ISEME TANI 2000 ZA KOROSHO ZA WAKULIMA WA KUSINI ZIMEPELEKWA WAPI ?

Anaandika Juma Polle, Mheshimiwa Diwani wa Mijelejele....

Serikali inapaswa kutuambia kwa kina tani 2000 za korosho zilizopotea katika ghala kuu la BUCO zimekwenda wapi na kachukua nani ilihali WHR (Where house) zinaonyesha korosho zilipokelewa na kwanini taharifa izi wanazificha kutaka kuwa siri..

pili, Juzi tumemsikia kaimu meneja wa Mamcu akisema korosho ambazo azijalipwa mpaka sasa zitalipiwa kwa bei ya 2800/= ni kigezo kipi anachotumia kupanga bei hiyo ilihari sote tunajua mnada wa tarehe 7/11/2016 uliuzwa kwa bei ya 3760/= ambao nao mpaka leo hii aujalipwa kwa mkulima na pia mnada wa tarehe 1/11/2016 korosho ziliuzwa kwa bei ya 3757/=

 Ifike wakati tuwe wazi tusitumie mwamvuli wa chama tawala kujirindia na maovu. Nilitegemea kusikia kauli za wateule wa mh rais juu ya ili swala, Uku vijijini njaa imeshaanza kufukuta na pia kuanzia tarehe 9/1/2017 shule zinafunguliwa na mpaka sasa wakulima wameshindwa kuwaanda watoto wao kwa kuanza mwaka mpya wa masomo kutokana na kukosa fedha.

                         BELIEVE IN TOMORROW

Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments:

  1. big up mkuu kwa kutupa habari mpya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Endelea kuungana nasi uweze kupata habari mbalimbali kila siku

      Delete