Serikali ya awamo ya Tano imejikita katika sekta ya elimu kuhakikisha Wananchi na watanzania kwa ujumla wanapambana kwa nguvu zote kuhakikisha wanamtokemeza adui Ujinga. Kwa msingi huo Serikali Ya Tanzania chini ya rais wake J. Pombe Magufuli wamefuta gharama za Uchangiaji kwa elimu ya Kiwango cha Kidato cha nne (4).
Kwa kuliona hilo Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Masasi ndugu DR Rashidi M. Chuachua kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Masasi kupitia idara ya Ustawi wa jamii. Imeendesha zoezi la kugawa Uniform na Vifaa vingine muhimu katika mchakato wa kujifunzia kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu na mayatima.
Mwandishi wetu alipata nafasi ya kuzungumza na Afisa Ustawi wa Jamii wa Hamashauri ya Mji wa Masasi alikuwa na haya ya kusema:
" kwa jina naitwa Mariamu Kawambwa ni afisa ustawi wa Jamii Halmashauri ya mji wa Masasi. Leo tupo katika zoezi la kugawa uniform na vifaa vingine vya shule kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na mayatima katika kata 14 za halmashauri ya mji wa masasi. Zoezi hilo limeusisha shule 8 za Kata ya Masasi. Shule zilizonufaika na Zoezi hilo ni kama ifuatavyo : -
1. Shule ya Sekondari Nangaya
2. shule ya Sekondari Mtapika Day
3. Shule ya sekondari Sululu
4.Shule ya Sekondari Masasi Day
5. Shule ya Sekondari Anna Abdallah
6. Shule ya Sekondari Mpindimbi
7. Shule ya Sekondari Marika
8.Shule ya Sekondari Mtandi
Hivyo, Zoezi limegharimu takribani shilingi 2,600,000/= Wanafunzi takribani 55 wananufaika na zoezi ili linaloendeshwa na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Masasi ndugu Dr Rashid M. Chuachua. Pia kuna wanafunzi ambao wananufaika na Zoezi hili lakini wapo nje ya halmashauri ya mji wa Masasi lakini kigezo ni wakazi wa ndani ya kata za Hamashauri ya mji Masasi na Wanaishi katika mazingira magumu. Mmoja yupo Chuoni Cha Utumishi Mtwara ngazi ya certificate, Pia mwingine yupo Kidato cha Tano Shule ya Lindi Sekondari na wa Mwisho Yupo Songea."
Pamoja na kufanikiwa kwa zoezi hili la ugawaji wa vifaa lakini kuna Changamoto zilijitokeza miongoni mwa Changamoto ni usafiri kushindwa kupata gari kwa muda uliopangwa sababu ambayo ilipelekea kuhahirishwa mara kadhaa kwa zoezi hili pia changamoto nyingine kubwa ambayo imejitokeza ni kutoripoti kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2017 katika shule walizopangiwa. Ofisi ya Mbunge Kupitia Katibu wa Mbunge ndugu Alfred Mrope anafatilia wanafunzi wasiolipoti shule kwa wazazi wao hili kujua tatizo hasa ni nini kilichofanya washindwe kuripoti?
Miongoni mwa Vifaa ambavyo wamekabidhiwa ni kama inavyoonekana katika orodha hii hapa chini.
Miongoni mwa Vifaa ambavyo wamekabidhiwa ni kama inavyoonekana katika orodha hii hapa chini.
Amekabidhi:-
1. Daftari Dozen 2 kwa kila Mmoja
2. Makebe (mathematical set yenye pen na pencil)
3. Begi la kubebea daftari
4. Sare (Uniform)
5. Viatu na Soksi
2. Makebe (mathematical set yenye pen na pencil)
3. Begi la kubebea daftari
4. Sare (Uniform)
5. Viatu na Soksi
Lengo letu watoto hawa wasome wakiwa na mazingira mazuri yanayofanana
na wenzao wanaotoka kwenye familia zenye uwezo na kukiwekeza kwenye
Elimu ina maana tumeikomboa jamii kwa kuwaelimisha.
Uongozi ni mipango na mikakati katika kuikomboa Jamii, tusaidiane kuelimisha Jamii....
Pia nichukue fursa hii kuwapongeza Maafisa Maendeleo wa Jamii kwa kushirikiana nasi kuwapata watoto hawa wanaohitaji Jamii iwasaidie.
Pia nichukue fursa hii kuwapongeza Maafisa Maendeleo wa Jamii kwa kushirikiana nasi kuwapata watoto hawa wanaohitaji Jamii iwasaidie.
Zoezi hili litakuwa endelevu kwa kipindi cha miaka 5 likiwa chini ya Usimamizi wa Ofisi ya Mbunge wakishirikiana na Halmashauri ya mji wa Masasi.
Maendeleo Ya Masasi Yataletwa kwa Ushirikiano wa mimi, wewe na yule.
07.02.2017
Masasi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpindimbi wakipokea uniform na vifaa vingine vya Shule kutoka kwa Katibu wa Mbunge Alfred Mroepe.
Katibu wa Mbunge Pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamiii wa Halmashuri ya mji Masasi wakishusha Vifaa katika Shule ya Sekondari Nangaya.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nangaya Wakipokea vifaa na Uniform kutoka kwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Masasi Ndugu Dr Rashid M. Chuachua.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtapika Day wakipokea vifaa vya shule pamoja na Uniform kutoka kwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Masasi.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji Masasi. Bi Mariam Kawambwa akiwa Ofisini kwa Mkuu wa Shule ya Sekonndari Mtandi akifanya taratibu za Kiofisi kwa ajili ya kuanza zoezi la Kugawa uniform na Vifaa na Vifaa vya Shule.

0 comments:
Post a Comment