Mahakama ya juu nchini Korea Kusini imeunga mkono uamuzi wa bunge wa kumuondoa rais wa taifa hilo Park Geun-hye mamlakani.
Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia.Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.
Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yalio na wapinzani wa rais huyo.
Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.
Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60.
- Rais wa Korea Kusini tayari kujiuzulu
- Wabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini
- Rais wa Korea Kusini alinunua dawa za Viagra
Bi Park alikuwa amesimamishwa kuhudumu kama rais tangu mwezi Disemba huku waziri mkuu wa taifa hilo akichukua majukumu ya kuongoza taifa.
Bi Choi wakati huohuo ameshtakiwa kwa kuchukua hongo kwa madai ya kuyashinikiza makampuni makubwa kumpa pesa huku akiahidi kwamba kampuni hizo zitapendelewa na serikali.
Bi Park ameshtumiwa kwa kushirikiana na Choi.
Jopo la majaji wanane katika mahakama ya kikatiba liliangazia mashtaka yanayomkabili bi Park na kuamua kwamba kulikuwa na sababu mwafaka za kumwachisha kazi.
0 comments:
Post a Comment