mwanazuoni

AHADI YA MAVUGO KWA MASHABIKI WA SIMBA SC

MSHAMBULIAJI tegemeo wa Simba Laudit Mavugo, ametuma salam katika kikosi ya Kagera Sugar kwamba lazima awafunge ili kuendeleza moto wake wa upachikaji mabao katika ligi kuu.
Mchezo huo ni kati ya michezo mitatu ambayo Simba itacheza Kanda ya Ziwa katika kipindi cha wiki mbili. Baada ya mchezo wa kesho, Simba itaelekea Mwanza Kuchezal na timu mbili za jiji hilo, Mbao FC na Toto Africans.

“Tumekuja huku (Kagera) kwa lengo la kushinda mchezo wetu na kupata pointi tatu muhimu, kama mshambuliaji kazi yangu ni kufunga na kusaidia timu kufanya vizuri,” amesema Mavugo.
Mshambuliaji huyo raia wa Burundi amesema kuwa pamoja na kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na wenyeji wao nao kuhitaji ushindi, bado anakipa nafasi kubwa kikosi chake kuibuka na ushindi.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment