mwanazuoni

Hizi ndio sababu kwanini Ferguson anatajwa kuwa ndio alimtengeneza Cr7 kuwa bora.

Kwa sasa Cristiano Ronaldo heshima yake ndani ya Real Madrid inapungua sana, halikuwa jambk la ajabu mtu kama Modrick kumfuata Zidane na kumuomba asimpange Ronaldo kwa kuwa kiwango kimeshuka. Lakini huyu Ronaldo ubora wake aliokuwa nao ana siri kubwa na Alex Ferguson na hii ndio siri kwanini Ferguson anatajwa kuwa mtu aliyemfanya Ronaldo aonekane bora.
1.Ronaldo alihitaji baba. Baba mzazi wa Ronaldo alikuwa aina ya mzazi ambaye alikuwa mlevi sana na mkorofi, unywaji pombe kali uliopitiliza ulimfanya apate ugonjwa wa ini ambao ulimuu na kumuacha Ronaldo akiwa na miaka 20. Baada ya hapo Ronaldo hakuwa na baba lakini. Ferguson alimlea Ronaldo kama mtoto wake na ikawa inamsaidia Ronaldo kupaona Manchester kama kwao, hata akiwa Madrid Ronaldo aliwahi kurudia kauli yake ya kusema “Ferguson ni kama baba yangu”
2.Ronaldo kwanza wengine baadae. Unamkumbuka Ruud Van Nisterlooy?unakumbuka alivyokuwa hatari katika ufungaji? Lakini Ferguson aliamua kumuuza Nisterlooy kwa kuwa aligombana na mwanaye (Ronaldo) mazoezini. Ferguson hakuwa anataka Ronaldo aguswe na ukimgusa tu ni sawa na kumgusa yeye, hii ikamfanya Ronaldo apambane zaidi kutokana na hili.
3.Fergie alimkuza Ronaldo siku ya kwanza tu klabuni. Wakati Ronaldo anakuja United alikuwa sio Ronaldo huyu japo alikuwa anajua mpira lakini sio kama hivi sasa, Ronaldo hakuwa anajiamini na aliwaza atapewa jezi namba 28 kama aliyokuwa akitumia alikotoka, lakini Fergie kuonesha imani yake alimpa jezi namba 7 ambayo hupewa wachezaji wenye vipaji katika klabu hiyo, jezi hiyo ilimfanya Ronaldo kujitahidi kuonesha alichonacho.
4.Alipewa nafasi ya kuonesha nini alichonacho. Staili ya soka la Ronaldo ilikuwa ni chenga nyingi na kasi, wengi hawakuamini kama anaweza kuwa aina ya mchezaji mkubwa United kutokana na aina yao ya uchezaji ambao hutawaliwa na nguvu, lakini Ferguson alimuacha Ronaldo kuwa huru na kuonesha nini alichonacho. Baada ya uhuru huo kilichofuatia ni rekodi, magoli na makombe, Ronaldo aligusa kila wavu wa wapinzani na kumfanya Ferguson atafune tu Big G na kutabasamu.
5.Mapenzi yaliyopitiliza. Katika mambo yote hayo kubwa lilikuwa ni mapenzi yaliyopitiliza kwa Ronaldo, Fergie alikuwa anamkingia sana kifua Ronaldo na ilimfanya Ronaldo kujiona mwenye bahati sana na kufanya kila analoweza kumfurahisha Ferguson na hii iliwafanya wapinzani wa United kuumizwa sana na Cristiano Ronaldo.

Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment