Naibu mshauri wa maswala ya usalama wa rais wa Marekani Donald Trump KT Mc Farland |
Naibu mshauri wa maswala ya usalama wa rais wa Marekani Donald Trump ameombwa na serikali hiyo ajiuzulu baada ya miezi mitatu pekee ya uteuzi wake kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Mc Farland ambaye aliwahi kuhudumu kama mchanganuzi wa kituo cha habari cha Fox News ametakiwa kuhudumu kama balozi wa Singapore badala yake kulingana na Bloomberg na Reuters.
Hatua hiyo inajiri baada ya Trump kumuondoa afisa wa mipango Steve Bannon katika baraza la usalama la taifa hilo.
Baraza hilo humshauri rais kuhusu maswala ya usalama wa kitaifa pamoja na maswala ya kigeni.
Uteuzi wa Banon mwezi Januari ulizua hofu kwamba swala la washauri wakuu lilikuwa likiingiziwa siasa.
Wachanganuzi wanasema kuwa hatua hiyo ya hivi karibuni inaonyesha kuwa mshauri mpya wa rais Trump kuhusu maswala ya usalama Luteni Jenerali McMaster analifanyia mabadiliko baraza hilo la NSC liliteuliwa na mtangulizi wake.
Aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Luteni Jenerali Michael Flynn alifutwa kazi baada ya wiki tatu na siku tatu pekee, baada ya kubainika alimdanganya makamu wa rais kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi nchini Marekani.bbc
0 comments:
Post a Comment