Jana jioni katika uwanja wa Bomani uliopo katika Halmashauri ya Masasi. Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Masasi Ndugu A. Mrope alikabidhi vifaa vya Michezo ikiwemo Jezi kwa Mwenyekiti wa Timu ya Silabu ndugu Frank Alfred akiambatana na Katibu wake Ndugu Yusufu Wema.
Timu ya Silabu ndio Mabingwa wa Ligi ya Mkoa wa Mtwara hivyo kwa sasa wapo katika Maandalizi ya kwenda kucheza katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa baada ya hapo kuanza kucheza ligi ya daraja la Pili.
Katibu huyo wa Mbunge alitoa salamu kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe: Dr Rashid Chuachua amabye yeye ananendelea na vikao vya Bunge mjini Dodoma pia anatarajia kuwasili Masasi kwa ajili ya kuupokea Mwenge siku ya tarehe 13.05.2017.
Maendeleo ya Sekta ya Michezo katika Jimbo la Masasi Yataletwa na wanaMasasi wenyewe kwa ushirikiano.
Michezo ni Fursa na Michezo ni Ajira.
Katibu wa Mbunge Akikabidhi Jezi |
0 comments:
Post a Comment