Kampuni moja ya data ya mitandaoni iliomfanyia kazi Donald Trump na ambayo ilitumika katika kampeni za Brexit sasa imeripotiwa kumfanyia kazi rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Kampuni hiyo iliokodishwa na kundi la kampeni za rais Trump imepongezwa kwa ushindi wa rais huyo.
Kampuni hiyo inanunua na kukusanya data kuhusu wapiga kura ikiwemo historia ya utumizi wao wa mtandao, mahali walipo pamoja na 'Likes' zao {wanachopenda} katika mtandao wa facebook.
- Rais Uhuru Kenyatta aionya mahakama
- Donald Trump na Uhuru Kenyatta wazungumza kwa Simu
- Uhuru Kenyatta: Vifaa vya uchaguzi vilikuwa vichache
Zinapochanganywa pamoja na utafiti unaofanywa , Cambridge Analytica inaweza kutumia data hiyo kutoa ujumbe muhimu kwa wapiga kura.
Kwa sasa Cambridge Analytica inafanya kazi Kenya , ikisaidia juhudi za kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru kenyatta.
Mnamo mwezi Mei , gazeti la The Star nchini Kenya liliripoti kwamba Chama cha rais Kenyatta, Jubilee kimekodisha kampuni hiyo , na mwezi mmoja baadaye ,gazeti hilo hilo liliripoti kwamba Cambridge Analytica ilikuwa ikifanya kazi katika ghorofa ya 7 ya jumba la makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi.
Cambridge Analytica ilikataa kutoa tamko lolote kuhusu ripoti hizo kwa kitengo cha habari cha BBC Trending, lakini shirika la Privacy International lilithibitisha kwamba liliona habari kama hizo katika gazeti la The Star kufuatia duru kadhaa, na kusema kuwa Cambridge Analytica inalipwa dola milioni sita kwa kazi yake nchini humo.
Cambridge Analytica ilishirikishwa katika siasa za Kenya 2013 wakati kampuni hiyo ilipomsaidia Kenyatta na chama cha National Alliance ambacho kilibadilika na kuwa Jubilee
Wakati wa kampeni za mwaka huo kampuni hiyo ilichanganya data ya mitandaoni na tafiti 47,000.
Kulingana na mtandao wa Analytica hatua hiyo iliisaidia kampuni hiyo kutengeza maelezo mafupi ya mpiga kura wa Kenya na kutafuta mikakati ya kampeni inayolingana na mahitaji ya mpiga kura mbali na hofu ya kuzuka kwa ghasia za kikabila.
Kenyatta alishinda uchaguzi huo wa 2013.
Wakenya ni miongoni mwa watu wanaotumia sana mtandao barani Afrika.
Idadi ya watu wanaotumia simu za rununu nchini humo iliongezeka kutoka watu milioni nane 2007 hadi milioni 30, 2013 na asilimia 88 ya idadi ya watu sasa wanaweza kutumia mtandao kupitia simu zao.
Baada ya kuhudumu kama waziri wa habari na mawasiliano kutoka 2005 hadio 2013 , Bitange Ndemo alikuwa mmoja wa viongozi waliosadia kupanua sekta ya teknolojia.
Aliambia BBC Trending kwamba mitandao ya kijamii ina jukumu kubwa katika kampeni za uchaguzi nchini humo.
''Inatoa njia ya haraka ya kujibu propaganda za mpinzani wako'' , alisema, mbali na kuwa mfumo wa mawasiliano unaoweza kuwafikia vijana wengi.
0 comments:
Post a Comment