Muungano wa upinzani nchini Kenya
National Super Alliance (Nasa) umeahirisha kikao cha kutoa tangazo
kuhusu mweleko wa chama hicho kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Kiongozi
wa muungano huo Raila Odinga alikuwa ameahidi kwamba angetangaza ni
hatua gani atachukua leo baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi
yaliyotangazwa Ijumaa, ambapo mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta
alitangazwa mshindi.Ajenti mkuu wa Nasa Musali Mudavadi amesema sasa muungano huo unapanga kutoa tangazo keshi Jumatano.
"Tunasikitika kwamba mashauriano yanachukua muda mwingi kuliko ilivyotarajiwa na Nasa kwa hivyo hawataweza kuwahutubia Wakenya kama walivyotarajia leo."
- Uchaguzi Kenya: Ni kwa nini Odinga hataki kwenda kortini?
- Upinzani Kenya wadai Odinga ndiye mshindi wa urais
Rais Kenyatta alitangazwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.
Hapo jana, Bw Odinga alikuwa ametoa wito kwa wafuasi wake kususia kazi kabla ya kutoa tangazo kubwa leo.
Watu wengi hata hivyo walionekana kupuuza wito wa kususia kazi.
Baada ya kutokea kwa maandamano katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi na mji wa Kisumu, hali ya utulivu ilianza kurejea Jumatatu.
Uchaguzi wa urais Kenya
Matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi
Tume ya uchaguzi ilisema mwanzoni ilikuwa haina taarifa kuhusu udukuzi kama huo lakini kwamba ingelifanya uchunguzi. Saa chache baadaye, tume hiyo ilisema hakuna jaribio lolote la udukuzi lililokuwa limefanyia katika sava ya matokeo ya uchaguzi.
Muungano wa upinzani pia umeikosoa IEBC kwa kutoa matokeo ya urais bila kuwasilisha fomu za kutangazwa kwa matokeo katika vituo vya kupigia kura na pia katika maeneo bunge, Fomu 34A na Fomu 34B.
Muungano huo umesema hautaenda kortini kupinga matokeo ya uchaguzi huo.bbc
0 comments:
Post a Comment