mwanazuoni

Kingwangala Aiagiza TAKUKURU Kuwakamata Waliotafuna Fedha za Ujenzi

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwakamata watu wote waliohusika kuchakachua fedha za ujenzi wa jengo la Zahanati ya Neruma.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara yake ya kuimalisha sekta ya afya wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo aliweza kukagua jengo  jengo la Zahanati ya Neruma,iliyopo Kata ya Neruma Wilayani Bunda, Mkoani Mara na kubaini milioni 29 fedha za ujenzi zikiwa zimechakachuliwa.

Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Isaack Mahela alimweleza Naibu Waziri kuwa, ujenzi wa jengo hilo umegharimu jumla ya milioni 29 kwa ajili ya kupanua na kuweka fremu za milango pamoja na madirisha, kitu ambacho kimeonekana hakiendani na uhalisia wa fedha hizo.

"Nakuagiza Mkurugenzi, uhakikishe unawasilisha nyaraka zote za fedha za jengo hili kwa TAKUKURU na wale wote waliohusika kupitisha fedha hizo na uwakabidhi TAKUKURU ili wafanye uchunguzi na kuchukua hatua zichukuliwe", amesema Dkt. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla amesema kuwa taifa linataka kusonga mbele hivyo watu wanaokwamisha mchakato wa Rais wa kuwaletea maendeleo wananchi wake lazima wachukuliwe hatua ili watu wengine waogope kutafuna fedha za umma.

Jengo hilo ambalo pia limeonekana kuwa chini ya kiwango katika maeneo kuta zake, mchakato wa ujenzi wa jengo ulianza tokea  mwaka 2015 kwa nguvu za wananchi na baadae Halmashauri ilitenga fedha za kumalizia mchakato kiasi cha milioni 29, ambazo zimebainika kutafunwa na watendaji waliokuwa wanashughulikia zoezi hilo.

Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment