Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan.
Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa kombora hilo limefyatuliwa kutoka maeneo ya karibu na mji mkuu wa Pyongyang.
Mwandishi wa BBC mjini Tokyo anasema kuwa kombora hilo lilipita anga za juu zaidi na kwenda mbali zaidi ikilinganishwa na kombora la awali.
Jaribio hilo linakuja siku chache tu baada ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani Rex Tillerson ametoa wito kwa China na Urusi kuchukuwa hatua za moja kwa moja dhidi ya Pyongyang, huku waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akitaja jaribio hilo la hivi punde kuwa ni kitendo cha kuudhi. bbc
0 comments:
Post a Comment