Kama ni mfuatiliaji mzuri wa soka la Bongo utakuwa unafahamu kuhusu historia ya mechi za Simba vs Toto Africans ya Mwanza. Toto imekuwa na rekodi ya kuisumbua Simba kila timu hizo zinapokutana kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara, mara kadha Simba imepata wakati mgumu kupata matokeo mbelea ya Toto iwe Mwanza au Dar.
Kuelekea mchezo wa Mbao vs Simba (Alhamisi September 21, 2017), nimemuuliza John Tegete kocha wa zamani wa Toto kama akipewa jukumu la kuwashauri benchi la ufundi la Mbao atawaambia wafanye nini ili kuhakikisha wanapata matokeo dhidi ya Simba.
Tegete amesema kinachohitajika ni benchi la ufundi kuwahamasidha wachezaji kabla ya mchezo na kuwajenga kisaikolojia ili kukabiliana na timu kubwa zenye wachezaji wenye majina.
“Kwanza inabidi kuhakikisha wachezaji wamehamasika vya kutosha kuelekea mechi kubwa kama hizi. Unawaambia ukweli kabisa hizi mechi ndio za kuwatoa, wanatakiwa kutulia na kucheza mpira bila kujali wanacheza na timu gani yenye wachezaji gani. Hizi ndio mechi za wao kujitangaza, wakifanya vizuri baada ya mechi wanaanza kutafutwa kwa ajili ya mipango ya kusajiliwa” Tegete.
“Bahati nzuri Mbao ni timu inayoundwa na vijana wengi ambao hawana majina, wana kocha mzuri ambaye anajua kufundisha na kujenga vijana kwa hiyo naamini kabisa mchezo wa kesho utakuwa mzuri kwa sababu Mbao wanakuja vizuri ukiachilia matokeo wanayopata.”
“Wachezaji wa Mbao hawapaswi kuangalia matokeo ya Simba waliyopata kwenye mechi zilizopita. Walishinda magoli saba kwenye mechi ya kwanza, mechi ya pili hawakufunga goli mechi ya tatu wakashinda tatu mbona hawakuendelea kushinda saba au zaidi.”
Kocha wa Mbao amesajili vizuri, anawachezaji aliowataka yeye ambao anajua wanaweza kupambana uwanjani kutafuta matokeo kwa ajili ya timu yao.
“Ukiangalia Liverpool walishinda 4-0 dhidi ya Arsenal lakini leo Liverpool wanapigwa kila kukicha kwa hiyo mchezo wa mpira wakati mwingine hatuangalii mambo yaliyopita tunaangalia mechi inayokuja.”
Tegete akatamba kwamba Simba hawamuwezi lakini ndio hivyo sisi makocha wengine tunafundisha huku kwenye timu zenye njaa lakini kama tunapata timu nzuri hakuna sababu ya kushindwa kufanya vizuri.
“Sisi makocha tunaofundisha timu hizi ndogo tupo bizuri sana ila watu hawajui, kinachotuponza sisi ni njaa, unafundisha timu wachezaji kupata tu chakula ni mmtihani bado mnasafiri bila pesa kwa hiyo tunashindwa kufanya vizuri kutokana na mambo mengi sio uwanjani tu.”
0 comments:
Post a Comment