Rais mpya wa Angola anatarajiwa kuapishwa leo Jumanne.
Hii ni mara ya kwanza kuna mabadiliko katika uongozi wa taifa hilo katika kipindi cha miongo karibu minne.
João Lourenço, aliyekuwa waziri wa ulinzi anachukuwa nafasi ya Jose Eduardo Dos Santos rais anayeondoka ambaye aliamua kuachia madaraka baada ya kuongoza miaka thalathini na nane.
Mwandishi wa BBC anasema japo watu wa Angola wanaunga mkono mabadiliko huenda kusishuhudiwe na mabadiliko makubwa kwa sababu
Bwana Lourenço amekuwa mwandani wa karibu wa chama tawala,MPLA(Popular Liberation Movement of ngola) kwa miongo kadhaa.
Dos Santos atasalia kuwa kiongozi wa chama hicho ambaye ana haki ya kuteua mkuu wa majeshi na polisi. Chama cha MPLA kimeongoza Angola tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ureno mwaka 1975.BBC
0 comments:
Post a Comment