mwanazuoni

Trump aishambulia Facebook.

Mkuu na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook ,Mark Zuckerberg, amebeza maoni ya rais Donald Trump dhidi ya mtandao huo kwamba umekuwa ukimpinga.
Zuckerberg amesema pande zote mbili za kisiasa nchini Marekani zilikuwa zikiutazama mtandao wa Facebook tofauti kutokana na kutofurahishwa na maoni yanayotolewa na watumiaji.
Ameongeza wakati wa uchaguzi Democrats wamewahi tuhumu mtandao huo kwamba unamsaidia Trump.
Mwanzilishi huyo wa Facebook amebainisha kuwa wakati wote wa uchaguzi mtandao wake ulifanya unachoweza kwa manufaa ya wapiga kura.
Hivi punde Facebook itawasilisha matangazo ya kisiasa 3,000 kwa wachunguzi wa serikali wanaochunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.
Mtandao huo unaamini huenda matangazo hayo yalinunuliwa na mashirika ya Urusi wakati na baada ya uchaguzi huo wa urais 2016.
Facebook, Twitter na Google imeombwa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya kijasusi ya bungela seneti Marekani Novemba 1 kuhusu tuhuma za Urusi kuwa na mkono katika uchaguzi wa Marekani.
Facebook na Google zimethibitisha zimepokea mualiko kuhudhuria kikao cha kamati hiyo, lakini hakuna katika mitandao hiyo iliyothibitisha kuwa itahudhuria.bbc
Share on Google Plus

. nyumbanitz

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment