mwanazuoni

ARIEL SHARON KUZIKWA LEO NA MAELFU YA WATU



Leo ni siku ambayo aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya Israel, aliyefariki siku ya jumamosi anatarajiwa kuzikwa leo baada ya maelfu ya watu wakitoa salamu zao za mwisho katika viwanja vya bunge la nchi mjini Jerusalem.
Sharon alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa kitandani kwa muda wa miaka nane huku akiwa anapumulia mashine.
Atafanyiwa ibada maalum ya kitaifa leo kabla ya kuzikwa karibu na shamba lake eneo la Sderot.
Waisreli pamoja na viongozi wa dunia, wametoa heshima zao za mwisho , lakini wale ambao wanaweza kusema hawajaguswa sana na kifo cha Sharon ni wapalestina.
Mwili wa Sharon ulifikishwa katika bunge la taifa Jumapili ambapo watu waliruhusiwa kuutizama siku nzima.
Maombi yalifanywa huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
Watu waliendelea kumiminika nje ya jengo hilo wengine wakiwasha mishumaa katika hatua ya kumuenzi Sharon.
Wageni mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria ibada maalum ya Ariel katika bunge la taifa wakiwemo makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, mjumbe maalum wa Mashariki ya kati Tony Blair, na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.
Sharon anakumbukwa na wengi kwa siasa zake na harakati zake dhidi ya wapalestina wakati akiwa mwanajeshi. Aliidhinisha ujenzi wa makazi ya walowezi katika eneo la Palestina na pia baadaye tume ya uchunguzi ilimpata na hatia ya kukosa kuzuia mauaji ya wapalestina yaliyofanywa na wakristo wa Phalangist baada ya Iisrael kuvamia Lebanon.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment