HALI YA ZITTO KABWE NI TETE
Akizungumza katika kipindi cha Baragumu kinachorushwa na televisheni ya Channel 10, Zitto amesema yupo tayari kupokea maamuzi ya kikao cha kamati kuu ambacho kitakaa kesho.japo anaonyesha maamuzi hayo yatakuwa siyo ya haki.
Zitto amekuwa mpole sana na anaonyesha kujua maamuzi ya kikao cha kesho kitu ambacho anasema yeye kama mwanasiasa lazima ajiandae kisaikolojia.
Ila amesema akishindwa kutafuta haki ndani ya chama basi atatumia katiba kupata haki.
Kesho kamati kuu itakaa kujadili kikao ambacho agenda zake zimewekwa hewani na Mkurungezi wa habari wa CHADEMA, pia kuna tetesi zinazosema kuwa pingamizi ya Zitto Kabwe kutupiliwa mbali na mahakama hivyo imewataka vijana wa chadema kutokea kwa wingi mahakamani kwenda kushuhudia kuumbuka kwa Zitto. Habari zaidi endelea kufatilia kupitia hapa.
.jpg)
Mtani
0 comments:
Post a Comment