mwanazuoni

KINACHOENDELEA BAADA YA BONGO MOVIE KUJIUNGA CCM

Jana katika mahadhimisho ya Chama Cha Mapinduzi kilipofanya sherehe ya kuanzimisha miaka 37 baada ya kuzaliwa kwake. kuna wasanii wa Bongo Movie kuchukua kadi na kuhamua kujiunga rasmi na chama hicho ambacho kinatawala lakini cha kushangaza wanaonekana kama wamekosea (pathema) kwa kitendo ambacho wamefanya katika nchi hii. Itambumbilike kuwa kila raia hana haki ya kuchiunga chama chochote ambacho yeye anakipenda. Kuna mambo yanaendelea katika mitandao ya kijamii baada ya wasanii hao kujiunga baadhi ya mambo hayo nia haya hapa japo kwa uchache.


Kinyume na hapo tunatambua haki yao ya kidemokrasia ya kujiunga na chama chochote na tunatarajia watambue haki yetu ya kidemokrasia ya kususia kazi zao kama tunavyo-protest against CCM na Makuwadi wao.

Haki yao ya kisiasa inalindwa kidemokrasia,haki yetu wateja wa kazi zao inalindwa na demokrasia ya mfumo wa soko huria.We'll exercise our democratic right.Wasitoe povu!

Protest inaendelea....

Operesheni Tokomeza unafiki na usaliti,Pambana kupigania mabadiliko kulinda Tasnia ya sanaa kwa maslahi mapana ya jamii

Wanasema Serikali ya CCM inaminya haki za wasanii kisera na kisheria,lakini leo wanaungana nao kuzuia mabadiliko ya kisera na kisheria ili wanufaike wote katika uboreshaji wa Tasnia ya sanaa

Wasanii wengi wamegeukia kujiuza na wengine wamegeuzwa punda(Drug Mules) kusafirisha madawa ya kulevya na kuliletea sifa mbaya Taifa kwa kuwa kazi zao hazilindwi kisera na kisheria ili ziwanufaishe.Leo hawakuangalia matatizo ya wasanii wenzao,wameangalia maslahi yao binafsi huku Tasnia hii ikididimizwa.Huu unafiki na usaliti haukubaliki

Comrade Julius umeua mno.Bado wanaweza ku-celebrate hapa na kudhani umewapa promo.Gosh....!

NDIYO RAHA YA DEMOKRASIA NA UHURU WA MAAMUZI, MSIWAONEE GERE!!

1. Chama walichojiunga ndicho kimepigania na kuboresha maisha ya wasanii wa Tanzania na leo wasanii hawana malalamiko yoyote, wanaishi raha mstarehe na kupata haki zote za msanii.

2. Kwa sababu ya CCM wasanii wetu wote wanafanya shoo zao ulaya na kupokea dolari na hata kwenda Mbeya kina JB ndiyo wameisaidia CCM kukata tiketi za ndege.

2. Kwa sababu ya CCM wasanii wa bongo ni matajiri kupindukia, kila mmoja anamiliki usafiri wa maana na ni hivi karibuni serikali itanunua helkopta za wasanii.

3. CCM imepigania na kutokomeza kabisa wizi wa mali za wasanii, ukipita Ubungo, Posta n.k. hakuna tena CD za kukopi za wasanii.

4. Baada ya miaka 50 ya uhuru msanii wa Bongo akiugua hatuhangaiki kumchangia akapate matibabu nje, mara zote wasanii hujitibu kwa mahela kibao wanayokusanya katika Shoo za Marekani, Ulaya n.k

5. Nami nawapongeza kina JB kwa kuchagua walipotaka ili wapate maisha bora, KWA KASI MPYA, NGUVU MPYA NA ARI MPYA.

Twallybu Ismaily
11 hours ago
WIVU WA CHADEMA

Kama kila mtu atajiunga chadema vyama vyote vitakwisha. Sasa JB na Mpoto kujinga CCM mmeumia sana. Naomba mjue hata Slaa ni CCM aliye ndani ya Chadema, maana kadi yake hajarudisha CCM. Pia, Mbowe ni CCM maana pesa alizopewa na Mb wa Mwibara ni kutoka ccm.

Chadema mlisha kosa credibility za kuongoza hii nchi. Na kama mtamtengemea huyo kikongwe wenu eti ndiyo anaweza kushika Dola mmechemsha. Naombeni muwatangulize wakina ZZK, Mnyika, Mdee lakini msije mkawaweke wakina Tundu na Lema, maana bado ubongo wao haujaweza kung'amua changamoto za kidemokrasia.
Napenda kusema Wasanii wanahaki ya kujiunga CCm kwa kuwa ndiyo chama chenye Demokrasia kwa kila mmoja.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment