UNAFIKI WA MHE. MBOWE KATIKA MAMBO MUHIMU
Kwanza kabisa napenda kuwashukuru wale wote ambao walitumia muda wao kupitia na
kudurusu makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho " WATANZANIA TUITAZAME
CHADEMA KWA JICHO LA TATU" Makala hiyo ilichapwa tarehe 12-02-2014 siku ya jumatano.
Ni makala ilichangiwa na watu wengi na kupokea maoni na ushauri kuliko makala zangu
zote ambazo nimewahi kuziandika hapo nyuma. Ila waswahili wanasema kuwa "kwenye
wengi hapakosi jambo" hivyo nilipokea maoni tofauti na ushauri lakini pia
nilipokea maneno yenye lugha chafu ila nimechukulia kama changamoto za walimwengu tu.
Mimi nasema kuwa wale wote waliotumia lugha chafu hawajui walitendalo na mimi
nimeshawasamehe.
Nimetoa utangulizi na sasa ni wakati mzuri kwenda kwenda katika kile ambacho
nimekusudia watu mbalimbali wapate kukijua japo kwa kutumia muda wao mchache katika
kudurusu haya machache ambayo ni mawazo yangu binafsi. Nasawishika leo kuandika
makala hii ambayo nitamzungumzia kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni pia ni
mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa kifupi CHADEMA.Kimsingi kuna
sababu mbalimbali ambazo zimenishawishi kuandika makala hii ila kubwa zaidi ni
mwenendo wa kiongozi wangu ambaye ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa kwa
wanajamii wa kitanzania, hivyo watanzania wezangu wasipomjua vizuri itakuwa ni hasara
kwa taifa kwani watajikuta wamepata hasara kubwa katika taifa ili masikini.
Kabla ya kuingia katika kusudio la makala hii ni vema kumjua japo kwa ufupi historia
yake kama ifuatavyo:
Jina lake ni Freeman Aikaeli Mbowe, amezaliwa 14 septemba, 1961 mkoani Kilimanjaro na
elimu yake ni ya sekondari tu kwani alisoma katika shule ya uhungo seminari iliyopo
Bukoba. pia ameoa mke ambaye ni mtoto wa mwasisi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
anayeitwa Lilian E. Mtei , Mhe. Mbowe amebahatika kuwa na watoto Sita na kwa sasa
anamke mwingine ambaye ni mke wa kisheria ambaye ni Joyce Mukya na kubahatika kupata
mtoto moja. Kuna watu watajiuliza Mhe. Mbowe ni mkristo itakuwa je awe na mke
mwingine hapa nitafafanua kwa uchache tu. Kumbuka sheria zinasema ukikaa na mwanamke
kwa miezi inayozidi sita unahesabika kuwa umeoa. Mhe. Mbowe bila ya kuhesababu huko
nyuma wamekuwa wapenzi kwa muda gani tuhesabu hapa kuanzia mimba mpaka kuzaa miezi
mingapi imepita ? je aijakamilika sita ya kisheria? najua kila mtu ambaye
atakishughulisha kichwa chake atakuwa amepata jibu la swali hilo.
Kwa sasa Mhe. Mbowe anajushughulisha na siasa pia ni mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo.
Mwaka 2000 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbola Hai ambalo alishinda kwa asilimia
64.5% za kura zote zilizopigwa, vile vile kutokana na ushindi ambao aliupata mwaka
2000 alitumia haki yake kikatiba na kujua kuwa watanzania wa Hai ni sawa na
watanzania wa nchi nzima akahamua kujitosa katika kugombea nafasi ya urais mwaka 2005
kukiwakilsha chama chake cha CHADEMA. Tarehe 14 Decemba, 2005 alipata asilimia 5.88%
ya kura. Baada ya matokeo hayo mimi kwa uwezo wangu nilijaliwa na mungu niliamini
kuwa mtoto akizaliwa uanza kukaa na kuendelea kutamba na mwisho kutembea lakini ni
tofauti na Mhe.Mbowe yeye alitambaa pia akatembea mwisho wa siku akarudia kutambaa
haya ni maajabu ya ulimwengu huu. hapa nina maana kuwa mwaka 2000 aligombea ubunge na
mwaka 2005 aligombea uraisi lakini cha ajabu mwaka 2010 alirudi kugombea ubunge kwa
mimi naona ni maajabu sijui wewe mwezangu? mwaka 2010 aligombea ubunge na kumshinda
mgombea wa CCM ndugu FUYI KIMBITA kwa asilimia 51.63% ya kura. hapa unaona ni jinsi
gani ameshuka kutoka asilimia 64.5 % mwaka 2000 na kufikia asilimia 51.63% matarajio
yangu mwaka 2015 atapata zile asilimia alizopata katika urais hii itatokana na
mwenendo wake wa sasa wa kiongozi huyu.
Baada ya kuwapatia machache na historia yake japo kwa ufupi ili wewe msomaji wa
makala hii uweze kujua ni nani anazungumziwa hapa na niwapi katoka mpaka kufikia hapa.
Swali ni kwa nini mwandishi wa makala amehamu kuandika hii makala yenye kitambulisho
cha " UNAFIKI WA MBOWE KATIKA MAMBO MUHIMU" kimsingi kuna sababu nyingi mno
zilizomshawishi mwandishi kuandika makala hii ila nitazitaja chache kutokana na wingi
wake ila mungu akipenda zitakuja kuzitaja nyingine katika makala nyingine pale tu
mwandishi atakapo pata wasaha wa kufanya hivyo, ila kwa uchache tujilizishe na hizi
zifuatazo:
A. UFISADI MKUBWA UNAOFANYWA NA MHE. MBOWE.
Mhe. Mbowe ni kiongozi mnafiki pale anapozungumzia suala la ufisadi kwa kuwa na yeye
ni fisadi mkubwa kwa msamiati huu niliupata kwa Bw Mengi ila mimi nitautumia kwa Mhe.
Mbowe kuwa naye ni fisadi papa. Hapa namnasibisha na Chui alivaa ngozi ya Kondoo.
Mhe. Mbowe ni fisadi papa na hapa nitaweka baadhi ya ithibati za kuthibitisha ufisadi
wake, kwa kuanza nitaanza na kumnukuu kiongozi mwenzie mwenye nafasi ya juu ndani ya
CHADEMA alipotamka haya maneno hivyo ni ithibati namba moja
" Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 ( Baada ya orodha ya mafisadi
kutangazwa2007)Mkono alimpa Freeman Aikaeli Mbowe shilingi Million 20 za uchaguzi
mdogo wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa "
Ni nukuu ya Zitto Kabwe katika profile yake ya Facebook.
Je huu si ufisadi? amepokea pesa kutoka kwa mtu kisha anakuja katika chama anasema
kuwa amekikopesha chama pesa na kushindikiza kulipwa na akalipwa huu ni ufisadi.
hivyo mtu huyu anapozungumzia ufisadi ni unafiki ulitukuka.
Pia chanzo cha taarifa kiliendelea kutoa data za ndani ambazo ni ithibati ya pili ya
ufisadi wa Mhe. Mbowe "Nadhani alimwambia pia mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe
Millioni 200 za kampeni ya Slaa pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Azizi alimpa
Mbowe Sh million 100 za kampeni. Lissu anajua ? "
Kwa maelezo hayo ya naibu katibu mkuu wa chama taifa ni ithibati tosha za
kuthibitisha kuwa Mbowe ni fiasdi papa ambaye ni mnafiki aliyetukuka na pale
anapokuwa anataka kuwaaminisha watanzania kuwaona kuwa CCM peke ndio mafisadi hali ya
kuwa naye ni miongoni mwa mafisadi huu ni unafiki uliyovuka kiwango yaani ni unafiki
ulitukuka. basi si hayo tu bali kuna ithibati nyingine ambayo inaonyesha kuwa
Mhe.Mbowe ni fisadi papa ni huu hapa chini ebu soma kwa makini halafu tafakari kwa
kina
" Kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Mhe. Mbowe alitufahamisha wanachama kuwa
alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa TSH 218.338,546. Mpaka sasa chama
kimekwisha mlipa TSH 175,000.000/= Baada ya kupata wadhifa wa makamu Mwenyekiti na
kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha
wilayani na makao makuu niliamua kumshauri Mbowe asitishe kujilipa deni kutokana na
fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopo kwa kuendana na utaratibu
wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.
Mhe. Mbowe alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibitishie
pesa hizo anazodai chama aliko[esha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya chama
yaani CHADEMA, KUPITIA HUNDI ipi na lini? nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha
chama kiilihidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa
maidhinisho ni dhahiri kuwa matumizi hayo haykuthibitishwa na chama na kwa mantiki
hiyo kuyafanya kuwa matuumizi binafsi ya Mhe. Mbowe. V ile vilenilimueleza kuwa
yalikuwa yakinukia harufu ya Ufisadi.
Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi
na au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii
kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana. nNa kwa kuwa hata baada ya
kuwa Mhe. mbowe amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopesha CHADEMA
VIFAA VYOTE YAKIWEMO MAGARI, VIPAZA SAUTI NA KADHALIKA VIMEBAKIA KUWA MALI YAKE
BINAFSI, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza
kitega uchumi cha watu binafsi. Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya
serikali, nilimuomba Mhe. Mbowe afuatilie kwa Msajili wa vyama kweli fedha za ruzuku
ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama
hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria. Nimesema kweli hapa
kwamba kwa wanachadema wengi walinichagua kuwa makamu mwenyekiti na hata mimi
mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi ya ubunge,udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka
2005 ningeferijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia
gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe
wote baada ya kulipa madeni kwa wateule wachache "
Je kuna shaka lolote nikisema kuwa Mhe. Mbowe ni fisadi papa ? hakuna shaka kwani kilakitu nimeweka wazi kupitia nukuu za viongozi wakubwa ndani ya chama cha
Demokrasia na Maendeleo. Kwa kudurusu baadhi ya maandiko tu hayo hapo juu tumeiona
ufisadi mkubwa unaofanywa na Mhe. Mbowe, swali la kujiuliza hapa tumempa taasisi
ndogo kama Saccos ameweza kufanya ufisadi wa kutisha kwa namna hii. Je, tukimpa nchi
au wizara ya fedha nchi itakuwa katika hali gani?
B. KUWAIBIA WANYONGE WA NCHI HII( UMMA UNATEKETEA KWA UNAFIKI WA MBOWE)
Napenda kuchukua nafasi adhimu ya kuwatazalisha ndugu zangu watanzania wezangu wenye
uzalendo na nchi hii kuwa makini na kiongozi huyu aliyevaa ngozi ya Kondoo angali
yeyey ni Chui mkubwa. Nchi hii ikiwa inajitaidi katika kupambana na maharamia wa
kigeni kumbe inasahau kuwa kuna maharami wanyeji ambao wamekuwa mwiba wa maendeleo ya
uchumi wetu ambao wanatumia nyadhifa zao katika kuwaibia wanyonge wa nchi hapa pia
nina mifano dhahiri ambayo ni ithibati tosha kuwa Mhe. Mbowe ni mnafiki katika mambo
muhiu ya taifa ili.
" aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kuifutia deni lake la NSSF. Aweke wazi mikataba yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas"
Ebu tazama ni jinsi gani huyu jamaa alivyokuwa nafiki ambaye hata athamini kazi
iliyofanywa na watanganyika walitukomboa katika unyonyaji wa watu weupe. Je maesahau
mchango wa wazee wangu hakina Abdulwahd Syjes, Osca Kambona,Bibi Titi Mohammed,J.K wa
Kwanza, Dossa Azizi, Mwalimu Kiyele,Mzee Mtevu na sheik Amiri na wengine wengi ambao
walitumia muda wao mwingi kuhakikisha mtanganyika anatoka katika unyonyaji wa namna
yoyote lakini leo mtanzania mwenzetu anaturudisha katika karne ya ukoloni kwa kutumia
rasilimali zetu kujinufaisha binafsi huu ni unyonyaji kwani NHC NA NSSF ni mali ya
wanyonge wa nchi hii. Pia kuwafanya watanzania kutopa mahitaji yao ya msingi kwa
kuendekeza tamaa zake ni kuwanyonya wanyonge wa nchi hii ebu soma hapa "
amemshinikiza mbunge wa viti maalumu ndugu Joyce Mukya, kukatisha ziara ya kikazi za
kibunge alipopangiwa na kumlazimisha wakutanane nyumbani kwake Dubai"
ushahidi wa ili ni hizi sms " bwana kabunju, salaam. Rejea mazungumzo kuhusu
Mhe.Joyce Mukya ambaye yuko safarini . Nitashukuru akibadilishiwa booking yake aweze
kuondoka New York Tarehe 1 Dec siku ya jumapili kurejea Dubai na kuunganisha Dar tar
3Dec. Mbowe,KUB.Cc Mhe.Joyce Mukya"
Huyu ni mtanzania mwenzetu ambaye anachukua mpaka kile kidogo chetu.
Pia wanyonyaji weusi wamekuja na mbinu mpya ya M4C yaani ni Movement for Change
ambayo kimsingi ni miongoni mwa mbinu ya unyonyaji kwa wanyonge wa nchi hii ambayo
mimi nainasibisha na mbinu zilizokuwa zinatumika katika kipindi cha feudalism
(ukabaila) pale Feudal lord(kwa sasa ni Mbowe) walipokuwa wanawatumia wakulima
katika kujipatia kipato chao bila hata jasho lakini leo hawa feudal lord wanawatumia
maskini wa nchi hii katika kujipatia kipato chao kwani tofauti ya feudal lord wa
karne ya 18's na hawa wa karne ya 21 ni moja tu kwani feudal lord walitumia
ardhi(land) lakini hawa wa sasa wanatumia M4C( Movement for Change ).
C. KUKIFANYA CHAMA KUWA MRADI WAKE BINAFSI
Mwenendo wa uendeshaji wa chama cha CHADEMA kwa sasa hakuna tofauti na uwendeshaji wa
biashara fulani nahisi sitokuwa nimekosea nikapo sema ni saccos kwa sababu mbalimbali
moja kuwa chama cha siasa kinaendeshwa kwa msingi wa kidemokrasia lakini saccos
inaendeshwa kwa msingi wa mmiliki je kuna tofauti na chadema ya Mbowe kwani yeye
anaiendesha jinsi anavyotaka. Hapa najua watanzania makini watakuwa wamenielewa kwa
wepesi kwani wengi wetu tunajihusisha na saccos pia nina ushahidi wa uwazishwaji wa
chama cha chadema. Ila kwa leo si lengo langu juu ya ili ilaitakapotakiwa nitakuja
kuchambua kila chama kilivyoanza ili watanzania wajue kwa nini nainasibisha CHADEMA
na SACCOS. Mhe. Mbowe amefanya chama ni mradi wake juu ya ushahidi wa ili nakuomba
rejea walaka wa Chacha Wangwe ambao umeelezewa katika hoja iliyopo katika kifungu "A"
cha makala hii.
D. KUTUMIA PESA NYINGI KUWATHIBITI WALE WOTE AMBAO NI WANADEMOKRASIA YA KWELI
Je Mhe. Mbowe si mnafiki? leo ukiniambia kuwa kiongozi huyu ni mzalendo na
mwanaDemokrasia napata mashaka na weledi watu ambaye atareta hoja ya namna hiyo kwa
sababu mbalimbali ikwemo juu ya mwenendo wake. Kuna mifano mingi sana ambayo
inathibitisha kuwa Mbowe si mwanademokrasia pia mnafiki aliyetukuka katika mambo
muhimu kwani ebu tureje mambo ambayo yamefanya Ndugu zangu Habibu Mchange, Mtela
Mwampamba, Samson Mwigamba,Dr Kitila Mkumbo,Marehemu Chacha Wangwe na Juliana Shonza
kuwa nje ya Chadema ? kuna watu watajito ufahamu kwa kufanya hawajui basi hata la
Mhe. Kafulila? sawa basi ili la juzi ambalo limefanywa kuwa kiboro la Mzalendo Zitto
Kabwe nalo tumelisahahu?
Nina mengi sana ila kwa kuwa muda na mambo ya kijamii yamekuwa nayo yakidai mudA
kutoka kwangu basi naoma nishie hapa ila natoa ahadi ya kuja kumalizia makala hii
wiki ijayo kwani itakua na muendelezo wa makala hii. Nakuomba msomaji wangu usikose
kusoma muendelezo wa makala hii.
Kwa maoni na Ushauri , tumia njia hizi za mawasiliano kwa mwandishi
Jina : MSHANA Junior
SIMU :0712 47 48 10
BARUA PEPE : halfanm8@gmail.com
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment