mwanazuoni

ZITTO KABWE ATOA YA MOYONI



Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujieleza kwa kushindwa kesi hadi kupoteza Sh340 bilioni za kodi ya ongezeko la mtaji katika uchimbaji urani.
 Juni 21, 2014 gazeti hili liliripoti hukumu ya kesi kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kampuni ya JSC Atomredmetzoloto (ARMZ) ikiituhumu kukwepa kodi ya zaidi ya Sh340 bilioni.
 Mahakama ya Rufani za kodi ilitupilia mbali madai hayo ikiipa ushindi ARMZ.
 Akizungumzia hukumu hiyo, Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema jana kuwa kukosa kodi hiyo siyo upungufu wa sheria bali ni uzembe wa Mamlaka ya Mapato na Wizara ya Nishati na Madini.
 “Habari ya Serikali kukosa Sh340 bilioni za kodi ya ongezeko la mtaji, imenigusa moja kwa moja kwa sababu mbili kubwa,” alisema na kuongeza:
 “Moja, Mwaka 2012 niliwasilisha muswada binafsi bungeni kurekebisha Muswada wa Fedha 2012 ambao ulikuwa unabadili Sheria ya Kodi ya Mapato 2004 kwa lengo la kuweka vipengele vitakavyowezesha nchi kupata kodi kutokana na mauzo ya kampuni za wawekezaji wanapouziana hisa au mali nje ya nchi.
 “Pili, mwaka 2013 niligombana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusu suala la kodi kutoka Kampuni ya Mantra Resources na Waziri alilihakikishia Bunge kuwa lazima kodi italipwa.  Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo wa TRA, Richard Kayombo alipoulizwa kwa simu jana alisema asingezungumzia suala hilo Jumapili na kwamba suala hilo bado lipo mahakamani.

Chanzo: Mwananchi.co.tz
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment