mwanazuoni

FREEMAN MBOWE MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA KWA MARA NYINGINE TENA

Freeman Mbowe akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.
Freeman Mbowe ameshinda tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa baada ya kupata jumla ya kura 789 huku mpinzani wake Ngambaranyela Mongatero akipata kura 20.



Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wakifuatilia mkutano huo.
Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Prof. Abdallah Safari aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za hapana zikiwa 34 baada ya kuwa mgombea asiye na mpinzani.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa Mohamed aliyepata jumla ya kura 645 huku mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph akiambulia kura 163
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment