ALI KIBA AMTAMBULISHA MPENZI WAKE
Fresh Jumbe aliwahi kusema penzi ni kikohozi kulificha huwezi.
Na sasa penzi la Jokate Mwegelo na Alikiba limefikia hatua ambayo haliwezi kuwa siri tena. Wawili hao wamekuwa wakidaiwa kuwa wapenzi kwa miezi kadhaa sasa lakini bado binafsi hawajeza kukubali wala kukataa.
Lakini sasa huenda hatua za awali za kuelekea kuuweka hadharani uhusiano huo zimeanza kufanyika. Alianza Jokate aliyepost selfie kwenye Instagram akiwa na msanii huyo aliyejipa jina la King Kiba na kutoandika chochote.
Naye Kiba jana alipost selfie nyingi kwenye akaunti yake ya Instagram na kuandika: Pop It In @jokatemwegelo #KingKiba.” Picha hiyo imevutia likes 8108 na comments 680.
Huenda picha hizo zikawa ni tangazo rasmi la uhusiano wao. Kuna tatizo moja lakini – Jokate aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond Platnumz!
0 comments:
Post a Comment