mwanazuoni

MVUMO WA MSHANA JUNIOR





" Hapa hatuchangui mtu maarufu, tunachangua mtu safi na huyu si safi" 1995
Nakumbusha Mshana Junior kuelekea uchaguzi mwaka huu . tusipime watu kwa kigezo cha sura bali tupime kwa kigezo za dhamira ya dhati na uadilifu na utayari wa kuwatumikia watanzania wanyonge na wakulima wa nchi hii.

" Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe na chai. wengine mnasema ahaaa ni tuhuma tu! lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipo tuhumiwa Ugoni, Kaisari akaagiza Uchunguzi ufanyike . uchunguzi ukafanyika na ikabahinika si kweli lakini Kaisari bado akamwacha , akasema mke wa kaaisari hapaswi hata kutuhumiwa."

Nakumbusha tu Mshana Junior tu kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu 2015.
Je wanaotangazia ni wasafi? pia hao watangaza nia hawajawai kutuhumiwa ? leo nawakumbusha tu hayo maneno ambayo yalitolewa mwaka 1995.

"sasa Tanzania inanuka rushwa ... tunataka kiongozi ambaye atasema rushwa kwangu mwiko.. mwaminifu kabisa kabisa hawezi kugusa rushwa..na watoa rushwa watamjua hivyo, lakini hatutaki aishie hapo tu, maana haitoshi wewe mwenyewe kuwa mwaminifu , unaweza kuwa mwaminifu kabisa lakini una shinikizo la ndugu zako, jamaa zako na marafiki zako."

nakumbusha Mshana Junior kueleka uchaguzi mkuu 2015.
Je wanaotangaza nia kweli wana uwezo wa kutogusa rushwa kabisa? je hao marafiki zao sio wala rushwa ? je ndugu zao wanamjua kweli kuwa yeye sio mla rushwa? Je ni mwaminifu kiasi cha kuwakemea hata wale ambao wanamchangia kiasi kikubwa cha pesa katika kufanikisha lengo na dhamira yake ya kuwatumikia watanzania?

Namaliza kwa kauli ya Mwl J k Nyerere ya mwaka 1995 katka kitabu chake cha "Nyufa" alisema hivi " Ikulu nimahala Patakatifu , mimi sikuchanguliwa na watanzania kuja kupafanya pango la Walaguzi na hakuna serikali yoyote duniani inayoongozwa bila miiko."

Asanteni sana ni kijana mpenda Maendeleo ya dhati kutoka kata ya Kawe. Tunaweza kuwasiliana kwa namba
0712 47 48 10
barua meme : halfanm8@gmail.com

chanzo cha baadhi ya maandiko ni hotuba za Mwl Jk Nyerere
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment