Hivi baadhi ya watu mnaposema Raisi Magufuli hajui lugha mnamaanisha nini? Mbona Maraisi na mawaziri wakuu kama wa Ujerumani, Japan, China, Norwei, Denmark, Finland, n.k. wanapoongea lugha za kwao hamuoni shida yoyote na hamsemi hawajui lugha? Ijapokuwa mimi najua kuwa Magufuli anajua Kiingereza sana tu kwani asingeweza kuandika tasnifu ya shahada ya juu kabisa ya uzamivu (Ph.D) kwa Kiingereza kama hakijui, lakini kuna shida gani akiamua kutumia Kiswahili kokote atakakokwenda halafu kuwe na mtu anayetafsiri kama wafanyavyo viongozi wa nchi nilizozitaja? Wenzetu wanajenga, wanatumia, wanasifu, na wanajivunia lugha zao, sisi tumebakia kukisifu na kukitukuza Kiingereza huku tukiidharau lugha yetu ya Kiswahili!! Tuache kasumba!!!
chanzo. Senkoro Femk
0 comments:
Post a Comment